30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Majanga mapya elimu, afya

Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki Elimu, John Kalaghe.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki Elimu, John Kalaghe.

Na Waandishi Wetu,

SEKTA za elimu na afya zinaonekana kukumbwa na changamoto mbalimbali zikiwamo mpya na hivyo kuzusha sintofahamu juu ya hatima yake nchini.

Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia katika shule za msingi na sekondari nchini umebaini zaidi ya asilimia 50 ya walimu hawafundishi.

Vilevile, sekta ya afya imekumbwa na changamoto mpya ambako kwa miezi kadhaa sasa chanjo mbalimbali zimeadimika zikiwamo za kichaa cha mbwa na pepopunda inayojulikana kama ‘tetenasi’ katika hospitali nchini zikiwamo za rufaa.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usomaji Duniani jana, Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki Elimu, John Kalaghe alisema utafiti huo ulifanywa kati ya 2014/15 na kuwasilishwa mwaka huu.

Hali hiyo imesababisha kushuka kiwango cha elimu katika shule za msingi na sekondari kutokana na walimu kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Utafiti huo unaonyesha zaidi ya asilimia 37 ya walimu waliokuwa shuleni hawakuingia darasani na  asilimia 17 ya walimu hawakufundisha kwa muda uliopangwa huku 14 hawakuwapo eneo la shule.

“Mwaka huu Benki ya Dunia imewasilisha ripoti yake ambayo inaonyesha   zaidi ya asilimia 50 ya walimu nchini hawafundishi, hawawajibiki na  wanashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo, jambo ambalo limesababisha kushuka   kiwango cha elimu,”alisema Kalaghe.

“Katika ripoti hiyo zaidi ya asilimia 40 ya walimu nchini hawana uwezo wa kufundisha, jambo ambalo linahitaji serikali kuongeza nguvu ya ziada  kuhakikisha wanawajengea uwezo walimu hao.

“Ili kuondokana na tatizo hilo serikali inapaswa kuboresha mazingira ya shule, kuongeza mishahara ya walimu kwa wale wanaostahili kulipwa vizuri  na kuwasimamia  waweze kuwajibika ipasavyo,” alisema Kalaghe.

Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Room to Read, Peter Mwakabwela, alisema   taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na serikali katika nyanja mbalimbali za utoaji wa elimu.

Alisema mpaka sasa wameweza kujenga maktaba katika baadhi ya shule na kuwajengea uwezo walimu wa darasa la kwanza na la pili ambao ndiyo msingi wa mwanafunzi kujua kusoma na kuandika.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Simbachawene, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda alisema licha ya serikali kuboresha sekta ya elimu, kunahitajika ushirikishwaji wa wadau mbalimbali   kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kukosekana kwa chanjo

Wakati huohuo, jana bungeni, Serikali ilikiri kuwapo   upungufu wa chanjo mbalimbali nchini.

Hata hivyo,    imekuwa na  kigugumizi kuzungumzia  chanjo ya kichaa cha mbwa ambayo inadaiwa kutokuwapo kwa muda mrefu katika hospitali karibu zote nchini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alitoa taarifa hiyo jana alipozungumza na waandishi wa habari   Dodoma.

Alizitaja chanjo zenye upungufu kuwa ni ile ya kukinga ugonjwa wa Surua na Rubella (MR), kifua kikuu (BCG), polio (OPV) na pepopunda (TT).

Ummy alieleza kuwa chanjo hizo zinatumika kwa watoto kuanzia wanapozaliwa hadi miaka miwili na wajawazito kulingana na mwongozo wa chanjo uliotolewa na wizara ili kuwakinga na magonjwa hayo.

“Ili kukabiliana na upungufu huu, wizara imekwisha kununua na inategemea kupokea chanjo za kukinga kifua kikuu (BCG)   dozi milioni 2 Septemba 28, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles