29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Wabunge CUF wamshukia Prof. Lipumba

Profesa Ibrahim Lipumba.
Profesa Ibrahim Lipumba.

NA RACHEL MRISHO, DODOMA

WABUNGE wa Chama cha Wananchi (CUF), wameshusha tuhuma nzito kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, wakidai kuwa amekula njama za kutaka kukivuruga kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, wabunge hao wamemtahadharisha Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kutokubali kutumika kukiyumbisha chama hicho.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge hao, Kiongozi wa Wabunge wa CUF, Riziki Shahari Mngwali, alisema Katiba ya CUF haitoi nafasi kwa kiongozi aliyejiuzulu kwa hiari yake kutengua uamuzi wake.

“Sisi kama wabunge na wawakilishi wa wananchi, tunatoa tahadhari kwa msajili wa vyama vya siasa na wale wanaotaka kutumika kukiingiza chama chetu katika mgogoro usiopaswa kuwapo.

“Msajili wa vyama vya siasa asikubali kujivunjia heshima yake kubwa akiwa jaji aliyehudumu katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa muda mrefu,” alisema Mngwali.

Alisema inadaiwa kuwa Profesa Lipumba na timu ya watu wachache wanaomuunga mkono, wameanza maandalizi mbalimbali ya kuchapisha fulana za kumpokea katika ofisi kuu za CUF Buguruni, Dar es Salaam muda wowote kuanzia sasa na kinachosubiriwa ni tangazo la msajili kuwa Profesa Lipumba ni mwenyekiti halali.

“Tunazo taarifa kuwa wanaandaliwa watu watakaovamia na kuiteka Ofisi Kuu ya CUF Buguruni, kufanya vurugu na kumsimika Profesa Lipumba kwenye nafasi ya uenyekiti na baadaye kusaidiwa kuzunguka nchi nzima kufanya vikao vya ndani ili kujaribu kuimaliza CUF, njama zote hizi tunazijua,” alisema Mngwali.

Alisema kutokuwapo kwa Profesa Lipumba ndani ya chama hicho hakujaathiri chochote, na kumshauri kuwa atulie kwani aliyokitendea chama hicho yanatosha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles