26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Majambazi wavamia gari la Magereza

Arodia Peter na Maneno Selanyika, Dar es Salaam

WATU wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamelishambulia basi la Jeshi la Magereza lenye namba za usajili MT. 0046 na kupiga risasi vioo vya basi hilo na kujeruhi watu kadhaa.

Waliojeruhiwa ni pamoja na askari magereza mwenye namba A9719 Sajenti Msofe pamoja na mahabusu mmoja ambaye hakufahamika jina lake.

Hata hivyo haikujulikana kama watu hao wamajeruhiwa kwa risasi au vioo vya basi hilo ambavyo vilikuwa vinaruka na kutawanyika ovyo.

Habari za kuaminika kutoka kwa watu waliokaribu na vyombo vya dola zililieleza MTANZANIA kuwa basi la Magereza likiwa na mahabusu 15 lilikuwa linatoka Mahakama ya Mwanzo Kawe kuelekea Mahakama ya Kinondoni kuchukua mahabusu na lilipofika karibu na eneo la Hoteli ya Regence lilipishana na watu wawili, mmoja akiwa ameshikilia kitu kama shuka akiwa ameficha bunduki aina ya shotgun.

Kamanda wa Polisi Mkoa

Basi la Magereza
Basi la Jeshi la Magereza lililoshambuliwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi

wa Kinondoni, Camillius Wambura, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema lilitokea saa 7 mchana jana, wakati basi hilo aina ya Isuzu lilipokuwa linatoka Mahakama ya Mwanzo Kawe kuelekea Kinondoni.

Alisema watu hao kabla ya kupishana na basi hilo walianza kurusha risasi na kujeruhi askari mmoja, dereva na mahabusu mmoja.

Alisema askari huyo alijeruhiwa vibaya na alipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, aliliambia MTANZANIA kwa njia ya simu kuwa majambazi hao walikuwa na lengo la kumdhuru mtu aliyekuwa kwenye gari lililokuwa mbele ya basi la Magereza na walipoliona gari hilo walifikiri kuwa lazima kutakuwa na askari mwenye silaha, lakini haikuwa hivyo kutokana na kwamba lilikuwa na watu wenye kesi ndogo hivyo halikuwa na askari mwenye silaha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles