25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Majaliwa: Tumieni bidhaa zinazozalishwa hapa nchini

Na Mwandishi Wetu

 Waziri Mkuu ametoa rai kwa taasisi zenye miradi mbalimbali nchini pamoja na wananchi kuthamini na kuzitumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini zikiwemo na za viwanda vya mkoa wa Pwani kwani zina viwango vya ubora.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumamosi Novemba 3, wakati akifunga wiki ya maonesho ya viwanda yaliyofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba katika kata ya Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani, ambapo amesema viwanda vilivyopo katika mkoa huo vimeudhihirishia umma kuwa vina uwezo mkubwa wa kuzalisha bidhaa zilizo bora na hata kuzidi zile zinazoingizwa kutoka nje, amewahamasisha wananchi kutumia bidhaa za ndani.

“Wakati natembelea mabanda kwenye maonesho haya nimeshuhudia bidhaa nyingi nzuri na zenye ubora. Nimeona wazalishaji wa saruji, mabati, nondo, marumaru, mabomba ya plastiki, chuma, zana za kilimo, vyakula, vinywaji na vifungashio,” amesema Majaliwa.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo ameiagiza mikoa yote nchini kuhakikisha inatumia bidhaa zinatengenezwa na viwanda vya ndani katika miradi mbalimbali ya ujenzi wanayoitekeleza kama ujenzi wa hospitali za wilaya na vituo vya afya.

“Wakuu wa Mikoa ni lazima hakikisheni bidhaa kama saruji, nondo, marumaru, mabati zinavyotumika katika ujenzi ziwe vimezalishwa na viwanda vya ndani kwa sababu vina viwango vya ubora unaotakiwa na pia itasaidia kuondoa tatizo la soko la bidhaa hizo,” amesema Jafo.

Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewataka watendaji wanaohusika na masuala ya viwanda kutoweka vikwazo kwa wawekezaji ambao wanakwenda katika ofisi zao kwa ajili ya kutafuta maeneo ya kuwekeza kwenye viwanda au wanaohitaji vibali kwani jambo hilo halina tija.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles