30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: Sijaridhishwa na gharama za ujenzi wa kituo cha afya Naipanga

Na Mwandishi Wetu, Lindi

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na gharama zilizotumika katika upanuzi wa kituo cha Afya cha Naipanga kilichopo Wilayani Nachingwea Mkoa wa Lindi na kusema kiasi cha shilingi Milioni 600 zilizotumika katika upanuzi wa kituo hicho hakiendani na uhalisia wa majengo yaliyojengwa.

Kufuatia hatua hiyo, Waziri Mkuu ameagiza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Dk. Charles Mtabho asihamishwe au kuondoka katika Wilaya hiyo hadi atakapokamilisha ujenzi wa majengo yote pamoja na baraza za kutembeza wagonjwa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu Oktoba 25, 2021) wakati akikagua mradi wa upanuzi wa kituo hicho cha afya pamoja na kuzungumza na wananchi katika muendelezo wake wa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Lindi.

Amesema Serikali imetoa muongozo katika maeneo yote yanayojengwa Vituo vya Afya kwa kiasi cha shilingi milioni 400 hadi 500 kituo kinakuwa kimekamilika kwa ujenzi wa majengo yote muhimu ikiwemo ujenzi wa chumba cha upasuaji, wodi ya wazazi, maabara, chumba cha kufulia nguo, chumba cha kuhifadhia maiti, kuchomea taka pamoja na nyumba za watumishi.

Awali akikagua Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari Maalum ya Wavulana ya Masomo ya Sayansi Waziri Mkuu ametoa pongezi kwa wananchi wa kijiji cha  Chiumbati kwa kujitolea eneo bure kwa Serikali ili kuwezesha ujenzi wa shule hiyo.

“Nawapongeza sana wananchi wenzangu kwa uzalendo mkubwa mliouonesha kwa Nchi yenu, kitendo hiki ni cha kuigwa na namna mnavyoendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kusogeza na kuboresha huduma kwa wananchi.

Awali, akitoa taarifa ya Utekelezaji wa ujenzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nachingwea Eng. Chionda Kawawa amesema mradi huo unatekelezwa kwa Ushirikiano wa michango ya wananchi, fedha kutoka Serikali kuu pamoja na Mapato ya ndani ya Halmashauri na awamu ya kwanza itagharimu Sh milioni 556.

Mradi huo hadi kukamilika kwake unatarajiwa kuwa na Madarasa 32, Nyumba za walimu 20, maabara za kemia, fizikia, baiolojia, mabweni 20 utaweza kuwahudumia wanafunzi 1600, kwa mgawanyo wa wanafunzi 800 kidato cha kwanza hadi cha nne na 800 wa kidato cha tano na sita mtawalia

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles