32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: Serikali itayafanyia kazi malalamiko ya ukaguzi Mirerani

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imepokea na itayafanyia kazi  malalamiko ya wabunge juu ya utaratibu  wa ukaguzi unaofanywa kwenye mgodi wa  Mererani,

“Nimesikia concern ya namna ukaguzi unavyoendelea pale katika mgodi wa Mirerani, nilipanga kutembelea Mirerani ili kuona hali hiyo na kutafuta ufumbuzi, nikuahidi Spika na waheshimiwa wabunge kwamba tumepokea na Serikali tutalifanyia kazi,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 29, 2021) bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka ambaye ambaye alitaka maelezo juu ya utaratibu wa ukaguzi katika mgodi huo. Mbunge huyo alikuwa akichangia mjadala wa hotuba makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini.

Amesema Serikali inapata fedha nyingi kupitia madini ya Tanzanite yanayochimbwa katika mgodi huo hivyo haiwezi kushindwa kununua mtambo unaoweza kufanya ukaguzi wenyewe bila kusumbua mtu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles