Na Mwandishi Wetu     |   Â
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema nyongeza za mishahara ya watumishi si lazima zitangazwe hadharani kwa sababu zina madhara yake.
Majaliwa ametoa kauli hiyo bungeni leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo (Chadema) ambaye  amehoji tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani haijawaongezea mishahara watumishi wa umma hivyo serikali haioni kufanya hivyo kama ni kukiuka sheria ya utumishi wa umma.
Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema watumishi wawe na imani na serikali kwa sababu inaoutaratibu wa kuwaongezea mishahara.
“Nyongeza za mwaka zile zinaendelea kutolewa, nyongeza za mishahara lipo na si zitangazwe hadharani kwa sababu huwa zinaleta athari maana gharama za bidhaa zinaweza kupanda na hata tunapolipa madeni huwa hatutangazi,”amesema Majaliwa.