31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

BULEMBO AMTAJA KIKWETE UUZWAJI SHULE YA WAZAZI

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA


MWENYEKITI Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo, amesema kuuzwa kwa Shule ya Sekondari Nyangao kunatokana na maelekezo yaliyotolewa mwaka 2013 na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete.

Taarifa iliyotolewa na Bulembo jana, ilisema shule hiyo ni miongoni mwa shule sita zilizouzwa kutokana na agizo la Kikwete.

Bulembo pia alikanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa mitandaoni zikisema kuwa alimuuzia shule hiyo Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa.

Alisema taarifa hizo zinazosambaa zina nia ovu ya kumchafua Waziri Mkuu kutokana na kazi ambazo amekuwa anazifanya kwa ajili ya wananchi wa Tanzania.

Bulembo alisema Kikwete aliagiza shule zinazomilikiwa na jumuiya hiyo zenye changamoto ziuzwe au ziingie ubia na ikishindikana zirejeshwe serikalini.

“Siku hiyo pia iliagizwa kuwa shule ya Kaole iliyokuwa ya jumuiya hiyo iliyopo Bagamoyo irudishwe katika Jumuiya ya Wazazi,” alisema Bulembo bila kufafanua shule hiyo ilikuwa chini ya nani wakati huo.

Aliongeza: “Utekelezaji wa maamuzi hayo ya jumuiya ulifanywa kwa kuzingatia taratibu na kuamuliwa na vikao halali ndani ya jumuiya na Baraza Kuu na Bodi ya Wadhamini.”

Bulembo ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kuteuliwa, alisema shule hiyo ilikuwa chakavu sana na Serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, iliifunga kutokana na kukosa sifa za kutoa huduma ya elimu.

Alisema mazingira hayo yalisababisha jumuiya kufanya maamuzi ya kuiendesha kwa ubia na baadaye iliposhindikana iliamua kuiuza kwa kufuata taratibu zote zinazohusika kisheria.

Alieleza katika vikao mbalimbali ikiwemo bodi yeye anaingia kama mwalikwa inapobidi na hakuna mali yoyote ya jumuiya ambayo alikuwa na mamlaka ya kiutendaji zikiwemo shule hizo.

Bulembo alisema taarifa za kwamba alishiriki kuuza shule hiyo ni upotoshaji.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles