29.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa ajitosa kumaliza makundi ya kisiasa CCM

 GRACE MACHA – ARUSHA 

WAZIRI Kuu, Kassim Majaliwa, amejitosa kumaliza makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi,(CCM) Jimbo la Arusha Mjini yaliyosababishwa na mnyukano wa wagombea wakati wakipambana kutafuta kuteuliea kuwa wagombea nafasi ya ubunge kupitia chama hicho. 

Hiyo imedhihiraka juzi wakati akizundua kampeni za ubunge jimbo la Arusha Mjini kwenye viwanja vya Relini, Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinama alihudhuria. 

Majaliwa aliwatambulisha wagombea 90 waliochuana na Gambo kwenye kura za maoni, huku akiwataka wanne walikuwa na ushawishi mkubwa kumuombea kura. 

Aliyepanda wa kwanza ni mfanyabiashara mashuhuri, Dk Philemon Mollel, maarufu Monaban ambaye aliwaomba wananchi wa Arusha kuchagua Rais mbunge na madiwani kutoka chama hicho, huku akitangaza kuwa hana ugomvi na Gambo hivyo wamchague. 

“Kuna baadhi ya watu wanasema mimi na Gambo hatupatani. Nataka niwaambie leo mimi na Gambo ni marafiki nawaombeni muichague CCM. Nawaombeni muichague kwa sababu ndiyo chama kitakachounda Serikali wakiwemo mawaziri, manaibu mawaziri , wabunge. Tutakapoichagua CCM ambayo inaongozwa na Dk. John Magufuli mniamini kabisa mtafaidi matunda ya serikali yenu,” alisema Monaban huku akishangiliwa. 

Meya mstaafu, Gaudence Lyimo, Meya aliyejiuzulu, Calist Lazaro na Wakili maarufu Albert Msando ambao wote walimuombea kura Gambo. 

GAMBO 

Gambo alimshukuru Rais, John Magufuli aliyedai ameendelea kuwa kiongozi na mzazi kwake kwani hata baada ya kuwepo kwa maneno mengi baada ya uchaguzi ndani, aliendelea kumuamini na kusimama naye. 

“Mheshimiwa Majaliwa mkuu nakushukuru wewe, namshukuru,rRais wetu kipindi cha mchakato wa uchaguzi na uteuzi kulikuwa na maneno mengi lakini Rais wetu alisimama imara na mimi sitamsahau kwenye historia ya maisha yangu. Atabaki kuwa rais wa historia ya maidha yangu binafsi lakini pia atabaki kuwa mzazi na mlezi wangu kwa sababu namna alivyosimama 

Aliahidi kushughulikia kero ya bei kubwa ya kodi ya pango wanayotozwa wafanyabishara waliopanga kwenye vibanda vya halmashauri ya jiji la Arusha kwa kile alichodai kuna maeneo wanatoza shilingi laki 5 kwa mwezi bei ambayo haiendani na hali ya biashara. 

“Nikiposikia tamasha la Safina limeahirishwa nilisikitika, nilifarijika kusikia na wewe kesho utaenda kushiriki. Nashukuru huo ni uungwana,” alisema Gambo. 

Majaliwa wataendelea kuwatumia wasanii kwenye mikutano yao licha ya baadhi ya wapinzani wao kuwabeza. 

“Mimi nashangaa , mtu anashangaa bila wasanii mkutano wa ccm haiendi. CCM inawaleta hapa kama watu waliowekeza kwenye muziki.tutaendelea kuwatumia wote nchini tutawapa fursa ya kufanya kazi na mtapata mapato yenu kupitia usanii wenu,” alisema. 

Alisema serikali itaanzisha bima kwa kila Mtanzania ambapo mchzkato wake utaanza rasmi kwenye kikao cha kwanza cha bunge endapo watachaguliwa. 

Kauli hiyo imeonekana ni kumjibu Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasiana Maendeleo, (CHADEMA), Tundu Lissu aliyeahidi kutoa bima kwa wananchi wote wakati akiongea na wananchi wa jiji la Arusha jumatatu wiki iliyopita. 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Zalothe Stephen alisema kuna kidudumtu kilipenyezwa kilipenyezwa wakati wa mchakato wa uteuzi wa wagombea kutaka kujua ni nani atateuliwa kugimbea jimbo la Arusha mjini lakini waliwapiga chenga ya mwili hawakuweza kujua mpaka alipotangazwa. 

 Mwenyekiti wa CCM, Arusha Mjini, Joseph Massawe alimhakikishia siku ya uchaguzi mpaka ifike saa 4 asubuhi Arusha itakuwa inaongoza kwa kura za ubunge na Urais. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles