27.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Majaji wastaafu Mahakama Kuu waagwa

Na Mary Gwera-Mahakama

Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Dk. Eliezer Feleshi amewahakikishia majaji wastaafu kuwa mahakama itaendelea kushirikiana nao katika masuala mbalimbali licha ya kuwa wamemaliza muda wao wa kazi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi wakati wa hafla fupi ya kuwaaga majaji wastaafu tisa wa Mahakama Kuu- Masjala Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi na Kazi, alisema utumishi uliotukuka wa majaji hao umesaidia kuleta ufanisi ndani mhimili huo.

“Napenda kuwapongeza kwa utumishi wenu uliotukuka kwa mahakama hadi kufikia siku ya leo, nipende kuwahakikishia kuwa mahakama itaendelea kuwa pamoja nanyi kwa kila hali, iwe kwa shida au raha,” alisema Dk. Feleshi

Kutokana na hali hiyo aliwataka majaji hao kutosita kushiriki katika shughuli mbalimbali za Mahakama ili kuendeleza maboresho ambayo Mahakama inakusudia kufikia kupitia mpango mkakati wake.

Kwa upande wake, Jaji Mstaafu  Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Fredrica Mgaya, aliushukuru uongozi wa Mahakama kwa kuwaandalia hafla hiyo kwani wao bado ni sehemu ya wanafamilia wa Mahakama.

Aliwataka watumishi wa Mahakama ambao bado wapo kazini kufanya kazi kwa bidii na kupenda kazi zao.

Majaji Wastaafu walioagwa ni pamoja na Sekieth Kihio, Projestus Rugazia, Augustine Shangwa, Laurence Kaduri, Gadi Mjemmas, Fredrica Mgaya, Ibrahim Mipawa, Aghaton Nchimbi pamoja na Pelagia Khaday.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles