NEW YORK, MAREKANI |
JUHUDI za Serikali ya Marekani katika kupambana na ugaidi barani Afrika zinakabiliwa na matatizo mengi, pengine hakuna kati ya hayo matatizo yanayokera, au kuwa hatarishi, na kumeendelea kuwapo hali ya magaidi wenyewe kuvunja ushirikiano na kukiuka malengo yao.
Hivi sasa mafungamano si kwa kikundi kimoja au itikadi moja, au wakati mwingine ni nani analipa zaidi. Hao wanaotekeleza operesheni za kigaidi wanaendelea kutokuwa wawazi na kukigawanya kikundi kimoja kutoka kingine.
Kwa mujibu wa maofisa wa ulinzi na usalama wa nchi za Magharibi na Afrika, ni kuwapo kiwango cha juu cha aina mpya ya wanaoendesha ugaidi, ambao wako tayari kushirikiana na vikundi vya kigaidi vyenye ushindani mkubwa kama vile al-Qaida na Islamic State, na wakati mwingine wanatumikia pande zote.
“Unahitaji kuwa na teknolojia ambayo inaweza kufuatilia mabadiliko haya na utalazimika kutopitwa na matukio ili kufahamu ni kikundi gani cha wapiganaji hao wana mafugamano na kikundi kingine,” Christopher Maier, Mkurugenzi wa kikosi cha kutokomeza ISIS ameiambia Sauti ya Amerika.
Maier ameongeza: “Kimsingi wanaungana na kuwaingiza wapiganaji mara kwa mara. Uwezo wa wapiganaji hao na viongozi wao unatumika kadiri watavyoweza kukidhi maslahi yao katika eneo walilokuwapo.”
Matokeo yake, katika matukio ya mashambulizi ya kigaidi ni vigumu sana kutambua nani ameyafanya shambulizi, ambapo baadhi ya mashambulizi yakiwa ni mchango wa vikundi zaidi ya kimoja.
Kutambua mashambulizi kama hayo imepelekea kuhitilafiana kati ya taasisi za Marekani zinazopambana na ugaidi na maofisa wake.