27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

PRESHA JUU CCM

Na MWANDISHI WETU


PRESHA juu CCM. Ndivyo unavyoweza kusema kwa sasa, wakati vikao vya juu vya maamuzi vya CCM vikitarajiwa kuanza leo jijini Dar es Salaam huku wingu zito likiwa limetanda kuhusu kada atakayerithi nafasi ya katibu mkuu wa chama hicho tawala.

Hatua hiyo imekuja kutokana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, kumwandikia barua Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Dk. John Magufuli, akimwomba kujiuzulu wadhifa wake huo.

Kinana ambaye amekuwa Katibu Mkuu wa CCM tangu mwaka 2012, taarifa ambazo gazeti hili limezipata kutoka katika vyanzo vyake na vile vilivyo karibu na mwanasiasa huyo, zinaeleza kwamba safari hii Rais Magufuli ameridhia ombi lake hilo baada ya kumkatalia mara mbili huko nyuma.

Julai 2016, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM ambao Rais mstaafu Jakaya Kikwete alimkabidhi uenyekiti wa CCM Rais Magufuli, ikiwa ni miezi minane tangu aingie madarakani, Kinana aliwasilisha barua ya kujiuzulu nafasi hiyo, lakini kiongozi huyo wa nchi aliikataa akimwomba amsaidie kwa sababu ya uzoefu wake.

Rais Magufuli, pia aliwataka manaibu katibu wakuu wawili na sekretarieti nzima ya chama hicho kuendelea na kazi.

Taarifa zinaeleza Kinana anatarajiwa kutangaza rasmi uamuzi wake wa kujiuzulu leo wakati vikao vya juu vya chama hicho kwa maana ya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) vitakapoanza kuketi, Ikulu, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika inaelezwa kuwa uamuzi wa Kinana kuomba kuondoka katika nafasi hiyo, unatokana pamoja na sababu nyingine, kuona yapo mambo ambayo hashirikishwi.

Inaelezwa miongoni mwa mambo ambayo Kinana anaona hakushirikishwa kwa nafasi yake na amepata kusikika akisikitika kwa watu wake wa karibu, ni suala zima la uundwaji wa kamati kuchunguza mali za CCM.

Tayari ripoti ya kamati hiyo ilikabidhiwa kwa Rais Magufuli hivi karibuni na kimsingi huenda ikajadiliwa na wahusika kuchukuliwa hatua katika vikao hivyo vinavyoanza kuketi leo.

Jambo jingine ni uteuzi wa wagombea ubunge katika majimbo ya Siha na Kinondoni, ambalo wana CCM wengi pia walilalamika kuwa utaratibu wa chama hicho ulikiukwa.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles