24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

MAHAKAMA YATUPA SHITAKA KUPINGA SHERIA YA HABARI

 

Na MASYENENE DAMIAN,

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza  imetupilia mbali kesi ya katiba iliyofunguliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kampuni ya Hali Halisi Publishers kupinga sheria ya huduma za vyombo vya habari.

Shauri hilo namba 2/2017 lilifunguliwa Januari 18, mwaka huu katika mahakama hiyo.

Lilikuwa likisikilizwa na Jaji Jacquline De-Mello ambaye amelitupilia mbali kwa vile  mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kulisikiliza.

Shauri hilo lilitajwa jana ili kutolewa uamuzi kwa mapingamizi matano yaliyowasilishwa na serikali Februari 10, mwaka huu kupinga kusikilizwa   shauri hilo.

Serikali lidai Mahakama hiyo haina uwezo wa kulisikiliza shauri hilo hivyo kuomba ilifute kwa gharama.

Akisoma uamuzi wa mahakama hiyo, Jaji De-Mello alisema shauri hilo linatupwa kwa sababu liko katika mahakama isiyo na mamlaka ya kulisikiliza.  

Akizungumza na MTANZANIA   nje ya mahakama jana,  Wakili wa walalamikaji, Edwin Hans alisema wao hawalalamikii uamuzi wa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ya kutunga kanuni za habari.

Alisema wanachopinga ni sheria ya huduma za vyombo vya habari iliyotungwa na Bunge.  

“Hukumu hii haina logic (mantiki) kabisa, sisi tunaipinga sheria hatupingi uamuzi wa waziri sasa wanavyotutaka twende ‘Judicial review’ hatuelewi kabisa.

“Judicial review unaenda ukiwa unataka kuomba kibali cha mahakama kutengua uamuzi wa mtu ama taasisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles