24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI WANASA MTANDAO WA WEZI WA BAJAJI

Na ABDALLAH AMIRI,

JESHI la Polisi wilayani  Igunga    limenasa mtandao wa wezi wa bajaji ambao wamekuwa wakipora na kusababisha mauaji ya madereva wake kwa   mwaka 2016 na mwaka 2017.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamisi Selemani Issa alisema katika uchunguzi   wa kina wamenaswa watu watutu ambao walikuwa wakijihusisha na matukio ya mauaji wa madereva wa bajaji na kuzipora.

Alisema tangu kuibuka matukio ya wizi wa bajaji mwaka jana, polisi walikuwa wakiendelea uchunguzi  kwa   miezi tisa na  juzi waliwakamata watuhumiwa watatu ambao ni vinara wa matukio ya wizi huo na mauaji.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Safari Anthoni (25), Safari Kija (22) ambao walikuwa madereva wa bajaji   na John Emmanuel (30), wote wakiwa wakazi wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

“Tuliwakamata watu hawa baada ya uchunguzi wa miezi tisa, tumewakamata huko Kahama mkoani Shinyanga na katika uchunguzi tumebaini kuwa ndiyo waliojihusisha na mauaji ya waendesha bajaji watatu wa Kata ya Igunga mjini,” alisema.

Alisema baada ya kukamatwa  watuhumiwa hao walifanya upekuzi majumbani kwao na kukuta wakiwa na bajaji tano,   kati yake tatu ni  za madereva wa bajaji waliouawa mwaka jana.

Bajaji tatu zilizotambuliwa ni zile zilizokuwa zikiendeshwa na Alex Okungu (30) aliyetekwa na kuuawa Agosti 16 mwaka jana, Songa Juma (24) aliyeuawa Desemba 10 mwaka jana na Maduhu Dwisha (35) aliyeuawa Machi 2 mwaka huu.

Polisi pia walikamata simu moja na kitambulisho, mali ya marehemu Maduhu Dwisha aliyeuawa Machi 2, mwaka huu na watuhumiwa walikiri kuhusika na matukio hayo.

  Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo alipongeza polisi kwa kufanikisha kupatikana kwa bajaji zilizoibiwa pamoja na watuhumiwa.

Alisema  matukio hayo yalikuwa yakisikitisha na kuwafanya wananchi kuilalamikia serikali.

Mwaipopo alisema kutokana na matukio hayo kushamiri,   aliagiza bajaji zote mwisho wa  kuendesha shughuli zake iwe  saa 1:00 usiku.   

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles