24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yaruhusu ushoga Uganda

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni

KAMPALA, Uganda

MAHAKAMA ya Kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, ambayo ilisababisha mataifa kadhaa ya magharibi kuinyima misaada.

Sheria hiyo ilizua mjadala si tu nchini Uganda bali kote duniani, kiasi cha kuyafanya mataifa ya magharibi yalazimike kuingilia kati.

Mahakama ilisema muswada uliopitishwa kabla ya kuidhinishwa na rais kuwa sheria ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao haikutosha kuupitisha na kwa hivyo ulikuwa kinyume na sheria.

Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja tayari vilikuwa vimeharamishwa nchini Uganda, lakini sheria hiyo mpya ilitoa adhabu kali zaidi.

Sheria hiyo iliharamisha hatua zozote za kueneza au kushawishi mapenzi ya jinsia moja na wakati huo huo ikiwajumuisha wanawake wasagaji katika kundi hilo.

Sheria hiyo iliyosainiwa na Rais Yoweri Museveni, Februari mwaka huu pamoja na mambo mengine inatoa adhabu ya kifungo cha maisha na inawataka Waganda kuripoti matukio ya kishoga au kisagaji kwa mamlaka husika.

Wabunge huenda wakalirudisha upya bungeni suala hilo, mchakato unaotarajia kuwa mrefu ukizingatia sheria ya sasa ilichukua miaka minne hadi kupitishwa.

Lakini wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wakisherehekea jana.

“Mimi si mhalifu tena, leo tumeandika historia kwa vizazi vingi vijavyo,” alisema Kasha Jacqueline, mmoja wa wanaharakati maarufu wa haki za mashoga waliofungua kesi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, alikuwa ameihusisha sheria hiyo na sheria za kifashisti za utawala dhalimu wa Nazi nchini Ujerumani.

Wakosoaji pia walidai Museveni aliisaini sheria ili kupata uungwaji mkono wakati wa kuelekea uchaguzi wa urais mwaka 2016, ambao utakuwa mwaka wake wa 30 madarakani.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Inasikitisha, kwa sababu ya umasikini nchi nyingi za kiafrika zipo tayari kukubali chochote zinachoambiwa na mataifa tajiri hata kama kipo kinyume na utashi/dhamiri yao. Chukua msimamo kama wa Mugabe, ni heri kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi ukiwa umepiga magoti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles