25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

MAHAKAMA YAOMBWA KUMFUTIA LEMA KESI ZA UCHOCHEZI

Na JANETH MUSHI -ARUSHA

WAKILI wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), Sheck Mfinanga, ameiomba Mahakama ya Wilaya ya Arusha kuahirisha kwa mara ya mwisho kesi mbili za uchochezi zinazomkabili mbunge huyo vinginevyo izifute.

Ombi hilo alilitoa jana mjini hapa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Devotha Msoffe, baada ya Wakili wa Serikali, Agness Hyera, kuiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi hizo kwa madai kuwa majalada yake yameitwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dare es Salaam

Jana mahakama hiyo ilipanga kumsomea hoja za awali mbunge huyo katika kesi mbili za uchochezi namba 440 na 441 za mwaka jana, lakini ilishindikana baada ya wakili wa Serikali kuieleza kuwa majalada hayo yamepelekwa kwa DPP.

Wakili Mfinanga alisema kuwa hiyo si sababu ya msingi kwa kuwa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na DPP, walikuwa wanajua nini wamepeleka mahakamani, hivyo huu si wakati wa kuangalia kama kuna kesi au hakuna.

“Tunaomba hili liwe ahirisho la mwisho kwa upande wa jamhuri, ‘other wise’ mashauri haya yafutwe, kwani ofisi ya DPP na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, walikuwa wanaleta nini mahakamani, huu si wakati wa kuangalia kama kuna kesi au hakuna,” alidai Wakili Mfinanga.

Awali aliiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo na kuipangia tarehe nyingine ya kuja kumsomea mshtakiwa huyo maelezo ya awali, kutokana na majalada hayo kuitwa kwa DPP.

Hakimu Msofe alikubaliana na ombi la Wakili Mfinanga na kuahirisha kesi hizo hadi Septemba 20, mwaka huu.

“Naahirisha kesi hizi kwa mara ya mwisho kwa upande wa jamhuri hadi Septemba 20, mwaka huu,” alisema.

Katika kesi namba 441, Lema anadaiwa kutoa matamshi yenye chuki na kuibua nia ovu kwa jamii.

Anadaiwa Oktoba 23 mwaka jana katika mkutano wa hadhara viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa, alitoa maneno: “Kiburi cha rais kisipojirekebisha, rais akiendelea kujiona yeye ni Mungu, mwaka 2020 haitafika Mungu atakuwa ameshamchukua maisha yake.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles