NA KULWA MZEE
-DAR ES SALAAM
JESHI la Polisi nchini linamshikilia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Lissu aliachiwa leo asubuhi na Hakimu Mkuu Mkazi, Huruma Shahidi baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Paul Kadushi kuwasilisha hati ya kuondoa shtaka hilo.
Kadushi aliwasilisha hati hiyo chini ya kifungua namba91 (1) cha makosa ya jinai akionyesha DPP hana haja ya kuendelea na kesi, mahakama ikaridhia na kumuachia.
Muda mfupi baada ya kuachiwa na kutoka nje ya mahakama alikatwa tena na askari waliokuwapo mahakamani hapo na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi.
Lissu alikuwa anashtakiwa kwamba Januari 11, mwaka huu katika kampeni za uchaguzi jimbo la Dimani aliwashawishi watu wasiridhike na wawe na nia ovu dhidi ya utawala.