28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mahakama yamwachia huru aliyemuua mbakaji wa mkewe

 ALLAN VICENT-TABORA

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora, imemwachia huru bila masharti yoyote mshtakiwa, Jumanne Nkuli, aliyekabiliwa na shtaka la mauaji baada ya kumkuta hana hatia.

Jumanne ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mahene wilayani Nzega, alikuwa anakabiliwa na kosa la kusababisha mauaji ya Mabula Ngassa, baada ya kumkuta akimbaka mke wake na alikiri mahakamani hapo kufanyakosa hilo ili kumtetea na alisababisha mauaji hayo bila kukusudia.

Akitoa uamuzi wa shauri hilo juzi baada yakusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora,John Utamwa, amemwachilia huru na kusema mahakama imeona kuwa mazingira ya mauaji yalitokana na mshtakiwa kukuta mkewe akiomba msaada wake kwa sababu alikuwa anabakwa.

Jaji Utamwa alisema mahakama imekubali maneno yaWakili wa utetezi, Chombala Kanani, kwamba mshtakiwa alisababisha mauaji hayo kwa kufanya kosa kubwa la jinai ambalo hata adhabu yake kisheria ni kubwa.

“Mshtakiwa alikuwa anachukua hatua ya kumlinda mkewe kwa kumtetea dhidi ya hatari aliyokuwa anakabiliana nayo ya kubakwa, kosaambalo lilikuwa linafanywa na watu ambao asingeweza kupima nguvu zao, mtuhumi waalitumia fimbo aliyoiokota eneo la tukio tena kwa kuirusha ikiwa ni njia yakujihami kwa kuzingatia kwamba ilikuwa ni usiku,” alisema.

Kabla ya uamuzi huo, upande wa Jamhuri ukiongozwa naWakili Tito Mwakalinga, ulidai Oktoba 12, 2016 mshtakiwa alisababisha kifo cha Mabula kwa kumpiga fimbo na kumsababishia majeraha mwilini mwake.

Wakili Mwakalinga alidai kuwa siku hiyo mshtakiwa aliporudi nyumbani kutoka katika sherehe ya harusi kwa jirani yao usiku alikuta mlango wa nyumba yake umevunjwa huku sauti ya mkewe ikisikika akiomba msaada.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles