26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 8, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MAHAKAMA YAMRUHUSU EKURU AUKOT KUGOMBEA URAIS KENYA

Mahakama Kuu nchini Kenya imemruhusu mgombea urais kupitia chama cha Thirdway Alliance, Ekuru Aukot, aliyekuwa ameshiriki uchaguzi mkuu tarehe 8 Agosti ashirikishwe kwenye uchaguzi mkuu mpya utakaofanyika tarehe 26 Oktoba.

Hapo awali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC) ilitangaza kuwa ni wagombea wawili pekee ambao ni Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee na Raila Odinga wa Muungano wa National Super Alliance (NASA) wangewania kwenye uchaguzi huo.

Hata hivyo, Raila Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi huo siku ya Jumanne.

Kwa upande wake, Dkt Aukot amesema amefurahia uamuzi huo na kwamba sasa watakuwa kwenye uchaguzi kwani Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alijaribu kuwafungia nje.

Ameongeza kuwa chama chake bado kina mambo ambayo kilitaka yashughulikiwe na tume hiyo ya uchaguzi tangu mwezi Agosti na bado hayajashughulikiwa.

Lakini pia amesema chama chake kitatoa maelezo ya kina kuhusu msimamo wao ndani siku mbili baada ya mashauriano zaidi.

Maafisa wakuu wa IEBC walikutana jana kutafakari kuhusu hatua za kuchukua baada ya hatua ya Odinga japo mpaka sasa bado hawajatoa tamko.

Pamoja na mambo mengine, kujumuishwa kwa mgombea huyo kuna maana kwamba IEBC haiwezi kumtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa moja kwa moja hata baada ya kujiondoa kwa Raila Odinga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles