25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yagoma kufuta dhamana ya Mdee,Bulaya

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetupilia mbali maombi ya
Jamhuri ya kutaka Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Bunda
Esther Bulaya wafutiwe dhamana kwa sababu haoni busara kufanya
maamuzi hayo.

Uamuzi huo ulitolewa jana jioni mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, baada ya kupitia hoja za pande zote mbili.

“Baada ya mahakama kupitia hoja inaona si busara kufuta dhamana kwa suala kama hilo, washtakiwa mkitaka kusafiri nje ya nchi muombe ruhusa,”alisema.


Hakimu Simba amekataa kuwanyang’anya washtakiwa hati za kusafiria kwa sababu pia si busara badi suala la msingi wawe wanaomba ruhusa.

Jamhuri katika maombi yao walitaka washtakiwa wafutiwe dhamana ama hati zao za kusafiria zishikiliwe huku wenyewe wakipinga kwa madai walienda Afrika Kusini kwenye matibabu baada ya kuomba ruhusa Mahakamani.


Mdee akijieleza alidai hali yake ya kiafya inafahamika Mahakamani na hata kuna wakati Hakimu Simba amekuwa akimuuliza anavyoendelea.

Anadai aliwahi kutoa taarifa za awali kwamba anakwenda kwenye matibabu wakati akiwa katika kesi nyingine namba 228 ya mwaka 2017 baada ya kubaini kwamba safari yake inaweza kuathiri kesi zote mbili.

“ Mheshimiwa hakimu nilitoa taarifa Novemba 25 na Desemba 18 mwaka jana , nilielekezwa kuandika barua ya ruhusa na nilipopata uhakika
wa lini naenda kupata matibabu, Januari sita daktari wangu wa Aga
Khan aliandika barua kwa Hakimu Mfawidhi.

“Daktari alieleza kwamba natakiwa kupata matibabu ya ziada nje ya nchi , wao kama hospitali ya ndani hawana uwezo huo, aliomba niongozane na Bulaya sababu anafahamika na madaktari ndani na nje ya nchi kutokana na mazingira ya matibabu yangu.


“Mama yangu mtu mzima, nilipopata barua tarehe saba nilimpa wakili wangu nikajiridhisha kwamba mahakama inayo taarifa ,”alidai Mdee
na kuomba kutoa vielelezo vya tiketi na hati ya kusafiria inayoonesha
kwamba Januari 10 mwaka huu alienda Afrika Kusini kwa kutumia ndege ya Shirika la Kenya na walipofika Kenya walihamia katika ndege nyingine iliyowafikisha safari yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles