28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Vifo virusi vya corona vyaongezeka, China ikiongeza vizuizi vya kusafiri

Beijing, China

CHINA imeongeza vizuizi vyake vya kusafiri katika jimbo la Hubei wakati vifo vinavyotokana na mlipuko wa virusi vya corona vikipanda hadi kufikia 26.

Vizuizi hivyo vitaathiri watu karibu milioni 20 katika miji 10, ikiwamo Wuhan, ambako virusi hivyo vilianzia.

Alhamisi,  mgonjwa mmoja aliyeathirika na virusi hivyo alifariki dunia kaskazini mwa jimbo la Hebei- na kufanya kuwa kisa cha kwanza katika eneo hilo.

Kifo kingine kilithibitishwa baadae kaskazini-mashariki mwa jimbo la Heilongjiang.

Jimbo hilo limepakana na nchi Urusi na ni umbali wa kilomita zaidi ya 2,000 kutoka Wuhan.

Nchini China hadi kufikia jana zilikuwa zimeripotiwa kesi 830 za wagonjwa walioathirika na virusi hivyo.

Kesi zingine ndogo zilizobainika nje ya China ni pamoja na Thailand, Marekani, Taiwan, Korea Kusini, Japan, Vietnam na  Singapore.

Uamuzi wa kuongezeka kwa vizuizi umekuja katika wakati ambao wachina wanajiandaa kusheherekea mwaka mpya maarufu kama ‘Lunar New Year’ moja katika shughuli muhimu katika kalenda ya China ambapo mamilioni ya watu husafiri kurejea makwao.

Wuhan huduma zote za usafiri wa mabasi, vivuko zimesitishwa ikiwamo zile za ndege na treni.

Wakazi wa maeneo hayo wameshauriwa kutoondoka huku barabara zikiripotiwa kuwekwa vizuiz.

Ezhou, mji mdogo wa jiji la Hubei, limefunga kituo chake cha treni wakati jiji la Enshi nalo limesitisha huduma zote za usafiri wa basi.

Majiji makubwa ya Beijing na Shanghai yamewaelekeza wakazi wote ambao wametokea katika maeneo yaliyoripotiwa kukumbwa na virusi hivyo kubaki majumbani mwao kwa siku 14 ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Mamlaka pia zimefunga vituo vikubwa vya kitalii ikiwamo Forbidden City cha Beijing na baadhi ya maeneo ya Great Wall.

Aidha wamefuta sherehe za umma katika baadhi ya maeneo ya kama yale ya ibada jijini Beijing na sherehe za kimataifa na kombe la mpira wa miguu la mwaka huko Hong Kong

Sherehe za mwaka mpya zote zimefungwa kwa muda Macau na Shanghai’s Disney Resort na migahawa ya McDonald’s katika miji mitano nayo imeathirika.

Wanasayansi wameweka bayana kwamba kila aliyeathirika na ugonjwa huo anaweza kusambaza kwa watu kati ya 1.4  na 2.5.

Awali, taarifa kutoka Kituo cha Tume ya Taifa ya Afya wakati idadi ya watu waliokufa ilipofikia 17,  kilisema mtu mwenye umri mdogo kabisa kufa kwa virusi hivyo ni yule mwenye miaka 48 na mkubwa ni wa miaka 89.

Waathirika wengi ni wale waliokuwa wanasumbuliwa na magonjwa sugu kama kisukari na Parkinson.

Wuhan ambako ugonjwa huo ulianzia ina jumla ya wakaazi milioni 11 na sasa mamlaka zipo kwenye mchakato wa haraka wa ujenzi wa hospitali itakayoingiza vitanda 1000  ili kushughulikia waathirika wa ugonjwa huo

Mkakati huo umekuja baada ya malalamiko mengi kutoka kwa wakazi wake ya kupanga foleni ndefu kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa ugonjwa huo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) haijaweka ugonjwa huo  kwenye ngazi ya dharura kwa sababu ya idadindogo ya watu walioripotiwa kuathirika hadi sasa.

“Bado haijafikia kiwango hicho,”  alisema Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus.

HALI ILIPOFIKIA

Alhamisi nchi za  Vietnam  na Singapore ziliingia kwenye orodha ya mataifa yaliyoripotiwa kukumbwa na virusi hivyo zikiungana na Thailand, Marekani, Taiwani na Korea Kusini.

Japan na Korea Kusini tayari zimethibitisha kisa cha pili.

Jana Singapore ilithibitisha kisa cha tatu cha mtoto wa mgonjwa aliyeathirika na ugonjwa huo huku Thailand ikiwa na wagonjwa watano hadi sasa

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles