24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama Maswa yawahukumu Viongozi wa AMCOS kwenda jela na kurejesha fedha zilizopotea

Na Samwel Mwanga, Simiyu

MAHAKAMA ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imewakuta na hatia Viongpzi watano wa Vyama vya Msingi wa Ushirika(AMCOS) waliokuwa wakikabiliwa na makosa mbalimbali katika mahakama hiyo.

Katika kesi ya Uhujumu Uchumi Na.1 ya mwaka 2022 iliyokuwa inamkabili, Samwel Makeja ambaye alikuwa Katibu wa Amcos ya Mbaragane amehukumiwa kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh 100,000 sambamba na kurejesha kiasi cha Sh 3,700,000 za Amcos hiyo.

Awali, mshitakiwa alikuwa akishitakiwa kwa makosa mawili ambayo ni Ubadhirifu wa fedha Sh 2,000,000 na kosa la Kuchepusha fedha za Amcos hiyo ambazo alipaswa kulipa Ushuru wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu(SIMCU) katika msimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2021/2022. Makosa hayo anadaiwa kuyafanya Oktoba 4 mwaka 2021.

Katika kesi ya Uhujumu Uchumi Na.2 ya mwaka 2022 iliyokuwa inamkabili, Gitulu Jayunga ambaye alikuwa Katibu wa Amcos ya Bugarama baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la Ubadhirifu wa fedha Sh 5,517,000 za Amcos hiyo amehukumiwa kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh 100,000 na kurejesha kiasi cha Sh 5,517,000.

Ilidaiwa fedha hizo alipaswa kulipa ushuru wa Chama Kikuu wa Ushirika mkoa wa Simiyu(SIMCU),Tume ya Maendeleo ya Ushirika(TCDC)na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika(COASCO) kwa musimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2021/2022.

Imedaiwa kuwa kosa hilo alilitenda Oktoba 7 mwaka 20221.

Katika kesi ya Uhujumu Uchumi Na.3 ya mwaka 2022  ilikuwa inawakabili, viongozi wa Amcos ya Iyogelo ambao ni Paul Hella ambaye ni Mwenyekiti na Daniel Bulabo ambaye ni Katibu kwa pamoja walishitakiwa kwa kosa la ubadhirifu wa fedha na hivyo kila mmoja alihukumiwa mwaka mmoja jela au faini ya Sh 50,000 na kwa pamoja warmerejesha kiasi cha fedha Sh 743,800 za Amcos hiyo.

Fedha hizo zilikuwa kwa ajili ya kulipia ushuru wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Simiyu(SIMCU),Tume ya Maendeleo ya Ushirika(TCDC)na Shirika la Ukaguzi wa Vyama Vya Ushirika(COASCO)katika musimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2021/2022.

Makosa hayo inadaiwa waliyafanya Oktoba 12 mwaka 2021.

Washitakiwa wote hao walikuwa wametenda makosa hayo ambayo ni  kinyume cha kifungu 28 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Sura 329 marejeo ya mwaka 2019.

Katika kesi ya jinai Na.68 ya mwaka 2022 iliyokuwa inamkabili Masishi Khija ambaye ni Katibu wa Amcos ya Isagenghe  alikuwa akishitakiwa kwa kosa la Udanganyifu wa fedha za wakulima kiasi cha Sh 106,150 .

Mshitakiwa alifanya kosa hilo kinyume na kifungu 304 cha kanuni ya Adhabu  sheria Na 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Katika shitaka hilo mshitakiwa alikiri kosa na mahakama kumpatia adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh 200,000 na kurejesha  kiasi cha fedha 106,150.

Washitakiwa wote walilipa faini na kurejesha kiasi cha fedha ambacho kila mmoja aliamriwa na Mahakama na wote waliachiwa huru.

Hukumu zote hizo zilitolewa na Hakimi Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Chirstian Rugumila huku upande wa Takukuru ukiwakilishwa na Mwendesha Mashitaka, Albertina  Mwigilwa akisaidiana na Mwendesha Mashitaka wa Serikali wa mkoa wa Simiyu, Rehema Sakafu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles