31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Waumini wa dini waombwa kuendelea kuiombea Nchi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waumini wa madhebu ya dini nchini waombwa kuiombea nchi ili kuepukana na majanga mbalimbali likiwemo la njaa, changamoto za kiuchumi zinazo sababishwa ama na binadamu au mataifa mengine, magonjwa, dhiki na mmomonyoko wa maadili.

Waziri George Simbachawene akiteta jambo na Mchungaji Fidelis Mngwabi (katikati) kabla ya ufunguzi rasmi wa sikukuu za vibanda (makambi) za kanisa la waadventista wa Wasabato Magomeni iliyofanyika Kwembe jijini Dar es Salaam.

Wito huo umetolewa leo Jumapili Agosti 14, 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene wakati wa ufunguzi rasmi wa Sikukuu za vibanda (makambi) za Kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni kwa Mwaka 2022, katika eneo la Kwembe jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na Kauli mbiu “NITAKWENDA KWA NGUVU ZA MUNGU”.

“Uwekezaji katika familia imara ni jambo la msingi, bila kwekeza katika familia hakuna nchi hakuna mataifa hakuna dunia. Msukumo wa watu wanaosimamia dhambi kutumia rasilimali fedha kwenye mambo maovu ni mkubwa kuliko msukumo wa kutetea mambo mema,” amesema Simbachawene.

Amefafanua kwamba pamoja na kumtegemea Mungu, bado maandiko matakatifu yanahimiza kufanya kazi kwa bidii.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene akipokea vitabu kutoka kwa Mchungaji Marko Barnabas, (kushoto) baada ya ufunguzi rasmi wa sikukuu za vibanda (makambi) za kanisa la waadventista wa Sabato Magomeni iliyofanyika Kwembe Jijini Dar es Salaam.

“Katika hili niendelee kuwasihi ndugu Waumini kufanya kazi kwa bidiii huku tukimtumainia Mungu na kuomba baraka zake katika kila kitu. Licha ya kwamba nchi yetu haiegemei upande wowote katika masuala ya dini (Secular State) lakini sehemu kubwa ya watu wake wanaamini katika Mungu kupitia dini na madhehebu mbalimbali.

“Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan inatambuamchango wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika sekta ya elimu kupitia taasisi zake za elimu; sekta ya afya kupitia hospitali na vituo vya afya; pamoja na sekta ya habari kupitia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa.

“Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa ustawi wa taasisi hizo ili ziendelee kuwa sehemu ya kuliletea maendeleo Taifa letu,” amesema Simbachawene.

Naye Mchungaji wa kanisa hilo, ambaye pia ni Askofu wa Jimbo la Mashariki Kati mwa Tanzania(ECT), Fidelis Mngwabi katika neno lake la shukrani ameishukuru serikali kwa kutambua mchango wa kanisa la Waadventista Wasabato katika kulinda umoja amani na upendo.

“Kanisa litaendelea kuwa na msimamo wa Mungu katika kusaidia waumini kwenda katika njia iliyo sahihi,” amesema Askofu Mngwabi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene akipanda mti baada ya ufunguzi rasmi wa sikukuu za vibanda (makambi) za kanisa la waadventista wa Sabato Magomeni iliyofanyika Kwembe Jijini Dar es Salaam.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles