26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli: Majangili wote wakamatwe

Rais Dk. John Magufuli akikagua meno 50 ya tembo yaliyokamatwa katika Operesheni Maalumu ya kukamata majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Dar es salaam jana.
Rais Dk. John Magufuli akikagua meno 50 ya tembo yaliyokamatwa katika Operesheni Maalumu ya kukamata majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Dar es salaam
jana.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli amekiagiza kikosi kazi kilichoundwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kuwakamata watu wote wanaojihusisha na ujangili bila kujali vyeo vyao, kabila zao au umaarufu wao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, kiongozi huyo wa nchi alitoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kushtukiza Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatilia utekelezaji wa operesheni ya kukabiliana na ujangili inayotekelezwa na kikosi hicho.

Pia aliwapongeza askari wote waliopo katika kikosi hicho na raia wema wanaotoa ushirikiano katika operesheni hiyo na kuwahakikishia kuwa anatambua kazi wanayoifanya na anawaunga mkono.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya na ninawahakikishia kuwa ninawaunga mkono, chapeni kazi, wakamateni wote wanaojihusisha na biashara hii haramu, hakuna wa kumbakiza, awe mkubwa au nani, kamateni, wala msijali cheo chake, umri wake, dini yake, kabila lake, umaarufu wake, sheria ni msumeno, watafuteni wote mpaka watu wakiona tembo wawe wanakimbia wenyewe ili tuokoe wanyama wetu wanaoendelea kutekelezwa.

“Hapa mmekamata pembe 50 maana yake tembo 25 wameuawa, haiwezekani maliasili yetu ikawa inapotea ovyo ovyo kwa sababu ya watu wachache wenye tamaa ya kutaka utajiri wa haraka haraka,” alisema Magufuli.

Akiwa wizarani hapo, Magufuli aliyekuwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudensi Milanzi, alishuhudia meno 50 ya tembo yaliyokamatwa Dar es Salaam juzi na jana.

Pia alionyeshwa magari yaliyokamatwa na kikosi hicho na watuhumiwa wanane wanaodaiwa kujihusisha na mtandao wa biashara haramu ya meno ya tembo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles