24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli kuzungumza na waandishi leo

RAIS Dk. John Magufuli
RAIS Dk. John Magufuli

Na Mwandishi Wetu – dar es salaam

RAIS Dk. John Magufuli, leo anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari Ikulu, Dar es Salaam.

Hii ni mara ya kwanza Rais Magufuli kuzungumza na waandishi wa habari tangu aingie madarakani Novemba 5, mwaka jana.

Katika mazungumzo ya leo, Rais Magufuli anatarajiwa kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ya kitaifa ambayo kwa siku za hivi karibuni yamekuwa yakilitikisa taifa.

Moja ya mambo hayo, ni maisha magumu na kilio cha wananchi kukosa fedha na tumbua tumbua majipu ambayo amekuwa akiifanya juu ya watumishi wa umma.

Pia katika mkutano huo, kuna uwezekano Rais Magufuli akazungumzia tuhuma nzito zinazowakabili wabunge wa CCM, ambao wanadaiwa kuhongwa Sh milioni 10 kila mmoja ili wapitishe Muswada wa Huduma ya Habari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles