29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

MAGUFULI AWATUNUKU KAMISHENI MAOFISA 165 WA JWTZ

Kamisheni na Rais Dk. John Magufuli Ikulu, Dar es Salaam jana. Picha na Silvan Kiwale

NA Aziza Masoud – Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli amewatanuku kamisheni maofisa 165 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliohitimu kozi ya cheo cha luteni usu baada ya kumaliza mafunzo Chuo cha Jeshi Monduli mkoani Arusha.

Tukio hilo lilifanyika Ikulu, Dar es Salaam jana na kati ya maofisa 180 waliohitimu mafunzo hayo katika kundi la 60/16  Watanzania walikuwa 165 na kati yao wanaume walikuwa 143 na wanawake 22.

Mafunzo hayo pia yalijumuisha wanafunzi wengine 15 kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki. Maofisa watano wametoka Burundi, watano wengine Kenya, Rwanda imetoa watatu na Uganda ikiwa na maofisa wawili.

Maofisa ambao si Watanzania  hawakutunukiwa kamisheni zao na Rais Magufuli kwa kuwa kwa utaratibu kila mwanajeshi anapaswa kutunukiwa na amiri jeshi mkuu wa nchi husika.

Rais Magufuli alifika katika viwanja hivyo saa 4:20 asubuhi na kabla ya kuwatunuku kamisheni hizo, alikabidhi zawadi kwa maofisa mbalimbali waliofanya vizuri katika mafunzo hayo.

Wanafunzi waliofanya vizuri katika mafunzo hayo ni pamoja na Said Iddy aliyetajwa kama mhitimu aliyefanya vizuri zaidi katika fani zote.

Zawadi ya mhitimu aliyefanya vizuri zaidi darasani ilienda kwa Shahari Ndabery wakati Hassan Mbaga alitajwa kufanya vizuri zaidi katika medani.

Mbali na hao, pia Rais Magufuli alitoa zawadi kwa Mariam Kayanda aliyefanya vizuri zaidi katika maofisa wanawake.

Pia alitoa zawadi kwa mwanafunzi aliyefanya vizuri kutoka nchi za nje ambaye ni Lucas Kisau kutoka Kenya.

Kabla ya kutunuku kamisheni hizo, Rais Magufuli alikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo hayo na baadaye akashuhudia burudani ya muziki wa bendi ya Mwenge na vikundi vya ngoma.

Akitoa historia fupi kuhusu mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli, Meja Jenerali Peter Massao, alisema maofisa hao walianza kozi ya Luteni Usuhiyo Februari 15, mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles