27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

MAGUFULI AONGOZA KUMUAGA MZEE MAJUTO, KUZIKWA TANGA


Elizabeth Joachim na Bethsheba Wambura,Dar es Salaam

MWILI wa msanii wa filamu za vichekesho, Amri Athumani kwa jina maarufu King Majuto unatarajiwa kuzikwa kesho mkoani Tanga katika shamba lake.

 

Mwili huo umeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam na idadi kubwa ya marafiki, ndugu, jamaa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Rais Dk John Magufuli ambaye alionyesha hisia zake kwa kutoa chozi.

Mzee Majuto amefariki dunia usiku wa jana majira ya saa mbili usiku kwa ugonjwa wa saratani lakini awali alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tezi dume.

Viongozi waliohudhulia kwenye kuaga mwili huo ni pamoja na Rais John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza.

Katika risala yake kwa wafiwa, Waziri Shonza amesema tasnia ya filamu na uigizaji imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na mtu muhimu na itachukua muda mrefu kupata mtu atakayeweza kuziba pengo lake.

“Sisi kama Wizara tumefanya jitihada ili kuhakikisha Mzee Majuto anabaki katika hali ya uzima lakini kwa kudra za mwenyenzi Mungu imeshindikana natoa shukrani zangu kwa Rais John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha amekuwa bega kwa bega nasi kwa kipindi tulichokuwa tukimuuguza mzee wetu” amesema Shonza.

Vilevile ametoa wito kwa makampuni yote ya matangazo ambayo mzee Majuto aliyofanyakazi nayo yatoe ushirikiano ili familia yake inufaike na kazi zake zilizobaki.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles