28.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli amng’oa Maswi TRA, atumbua wawili Uhamiaji

magufuriNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli amemrudisha Eliakim Maswi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara baada ya kile kilichoelezwa kukamilisha kazi maalumu aliyomtuma kuifanya katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kabla ya kurejeshwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Maswi aliteuliwa kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Desemba 30, mwaka jana.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, ilisema Rais Magufuli amefanya mabadiliko hayo kwa lengo la kumtafuta mtu mwenye utaalamu wa kuendeleza kazi iliyofanywa na Maswi.

Pamoja na hatua hiyo, pia Rais Magufuli amewasimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile na Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia utawala na fedha, Piniel Mgonja  ili kupisha uchunguzi kutokana na dosari alizozibaini Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alipotembelea Idara ya Uhamiaji hivi karibuni.

Balozi Sefue alizitaja dosari hizo kuwa ni pamoja na tuhuma za rushwa, ukusanyaji mbaya wa maduhuli ya Serikali, ukiukwaji wa taratibu za manunuzi na utendaji mbovu.

Alisema watendaji hao wakuu wa Uhamiaji wamesimamishwa kazi mara moja hadi hapo uchunguzi utakapokamilika na kwamba endapo watabainika kutokuwa na makosa rais ataamua hatma yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles