28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Magonjwa ya kitambi yanayowatesa wanawake

kitambiWIKI iliyopita tuliangalia homoni mbalimbali na madhara yanayoweza kutokea pindi inapotokea zimevurugika mwilini. Wiki hii tutahitimisha makala haya kwa kuangalia homoni zingine na makundi ya watu wenye ugonjwa huo.

Follicle Stimulating Hormon (FSH)

Hii ni homoni inayotolewa na upande wa mbele wa tezi ya ‘Pituitary’ kwenye ubongo baada ya kupata taarifa kutoka kwenye hypothalamus.

Homoni hii kazi yake kubwa huwa inakomaza mayai kwenye ovari za mwanamke. Kiwango hiki kinaonekana kuwa katika kiwango kidogo sana kwa mwanamke kwa sababu kiwango kingi cha estrogen kwenye damu kinapeleka taarifa kwenye ubongo kwamba homoni zipo zinajitosheleza na hatimaye ubongo hautatoa taarifa yoyote ya kutengenezwa kwa homoni hiyo.

Na hii ndio sababu kubwa ya ugumba kwa wanawake wenye PCOS (kitendo cha ovari kushindwa kutoa mayai kama kawaida) kwani kama hii homoni ipo katika kiwango cha chini hakuna yai lolote litakomazwa.
Homoni ya luteinizing (LH)
Homoni hii kwa wagonjwa huwa ipo pia katika kiwango cha kawaida au chini na hivyo basi inakuwa haiwezi tena kufanya kazi yake ipasavyo.

Kazi kubwa ya Luteinizing homoni ni kuishinikiza ovari itoe mayai kila mwezi yale yaliyo komaa.

Hivyo kama haifanyi kazi yake hakuna kitakachotimia katika zoezi zima la mayai kuja kwenye mirija ya uzazi kwa kurutubishwa.
Jinsi ya kubaini kama una ugonjwa

Wanasayansi hawakutaka kila mtu aje na tafsiri yake kwa ugonjwa huu, tunatumia ‘Rotterdam criteria’, huu ni mwongozo wa kuweza kubaini mwanamke kama ana ugonjwa huu au hapana. Mambo matatu muhimu katika ugonjwa huu.

  1. Dalili za magonjwa ya uzazi zote ambazo nimezitaja hapo juu.

 

  1. Kipimo cha damu na kwenda kuangalia homoni za Estrogen,Testosterone, FSH, LH na Insulin.
  2. Kipimo cha mionzi ya tumbo (Abdominal Ultrasound) ikinonesha ovari ina cyst nyingi (Polyfollicular ovary)

Endapo ukiangukia katika vitengo kuanzia viwili au vitatu basi kuna uwezekano mkubwa kuwa una ugonjwa wa PCOS.

Makundi ya watu wenye ugonjwa huu

Kundi la kwanza ni mwanamke ambaye amepima na kukutwa ovari zake zina ‘Poycysts’, hapati hedhi mara kwa mara yaani hedhi yake mbovu na ana dalili za homoni za kiume.
Kundi la pili ni mwanamke mwenye ovari zenye ‘Polycysts’ ana dalili za homoni za kiume lakini mzunguko wake upo vizuri, ana ndevu na ukipiga picha ya tumbo unakutana na ovari ina cysts. Ukimwambia una tatizo anakwambia ndevu za urithi, weusi huu shingoni ni wa urithi.

Kundi jingine ni mwanamke mwenye ovari zenye ‘polycysts’, hana dalili za homoni za kiume lakini mzunguko mbovu (huyu hana ndevu), hana dalili zozote za kiume lakini hedhi yake inamtia mawazo kila mwezi.
Kundi la mwisho ni wale ambao ovari zao zipo vizuri kabisa lakini ana dalili za homoni za kiume na mzunguko mbovu na wenye kuambatana na maumivu makali kupita kiasi.

Napenda kukupongeza kwa kufuatilia somo hili la afya ya mwanamke, makala zijazo nitazungumzia kwa kina namna ya kuondosha ugonjwa huu na jinsi gani vyakula tulivyozoea vinavyoangamiza afya yako.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles