Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Watoto wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Naiz Majani amesema Mafindofindo yasipotibiwa ipasavyo huleta maradhi ya moyo.
Dkt. Majani alisema kuwa mtoto anayeugua mafindofindo (tonsillitis) na kutibiwa kienyeji pasipo kufuata ushauri wa wataalamu yupo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya moyo siku zijazo.
“Tumegundua asilimia kubwa ya watoto wanaougua maradhi ya moyo sasa waliwahi kuugua mafindofindo na hawakutibiwa ipasavyo. Hivyo ni vyema umlete mtoto hospitalini mapema tumpime nakumpatia tiba sahihi ili kuwanusuru na maradhi mbalimbali,” alisema Dkt. Majani.