26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Madereva wapewa mafunzo ya usafirishaji salama kemikali hatarishi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Zaidi ya Madereva 100 wanaojihusisha na usafirishaji wa Kemikali na Mizigo Mingine Hatarishi nchini wamenufaika na mafunzo ya Usafirishaji salama wa kemikali mbalimbali yaliyotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Kanda ya Mashariki.

Mafunzo hayo yametajwa kuwa yatawasaidia kuzingatia kikamilifu sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na majumbani ya Mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2020.

Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias akikabidhi cheti kwa mmoja wa Madereva aliyeshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo madereva wanaoendesha Magari yanayosafarisha Kemikali na Mizigo Mingine hatarisha, mara baada ya kuhitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa TACAIDS kwa muda wa siku mbili.

Akifunga Mafunzo hayo yaliofanyika jijiniDar es Salaam katika ukumbi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAIDS), Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias amewataka madereva wote waliopatiwa mafunzo hayo, kuzingatia kwa uhalisia yale yote waliojifunza kuhusiana na usafirishaji wa Kemikali, ili kuweza kusafirisha salama kemikali hizo bila kujitokeza kwa madhara ya aina yoyote.

Mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa siku mbili yamehusisha mada mbalimbali kutoka kwa wataalam wa mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na taasisi nyingine za serikali ikiwemo mada ya sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani ya mwaka 2003.

Madereva wote walioshiriki kwenye mafunzo hayo wamepatiwa vyeti ambavyo vitaweza kuwatambulisha ushiriki wao kwenye mafunzo hayo, ambayo yametajwa kusaidia kuongeza idadi ya madereva wenye weledi wa usafirishaji salama wa kemikali na mizigo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles