25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Madaktari wa mifupa wapigwa msasa

Aveline Kitomary – Dar es Salaam

ZAIDI ya Madaktari Bingwa 50 wa mifupa kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ikiwemo Tanzania, wamepewa mafunzo ya upasuaji mifupa ya unyayo na kifundo cha mguu kwa njia ya kisasa zaidi.

Mafunzo hayo ya siku tatu yalitolewa na Taasisi ya Mifupa (MOI) ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Madaktari Bingwa  cha COSECSA na Chama cha Madaktari wa Mifupa nchini Uingereza (BOFAS).

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk Respicious Boniface, alisema taasisi hiyo imekuwa ikiwapatia wataalmu wake mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa lengo la kuwapa mbinu mpya ili waendane na  mabadiliko  ya teknolojia  ya matibabu yanayobadilika kwa kasi duniani.

“Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya afya hususani kwenye Taasisi ya MOI, hivyo ni jukumu letu kuhakikisha wataalam wanapata mbinu za kisasa zaidi ili waweze kuwahudumia wagonjwa vizuri na kupata matokeo bora  hivyo tunaendelea kuweka msisitizo kwenye mafunzo,”alisema Dk Boniface.

Pai alisema Serikali imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha fedha kuwapeleka wataalam nje ya nchi ili kupata mafunzo hayo hivyo kuleta wataalam nchini  kumeweza kuokoa fedha nyingi kwa nchi na nchi zingine.

 Kwa upande wake mkufunzi mratibu  wa mafunzo hayo  kutoka MOI, Dk Samwel Nungu, alisema washiriki wa mafunzo hayo wametoka katika nchi za Tanzania, Sudan, Zambi na Zimbabwe  huku lengo likiwa ni kuongeza ujuzi wa juu zaidi kwa Afrika.

“ Lengo letu ni kuunga mkono juhudi za serikali  kwa kuongeza idadi ya wataalmu  hivyo tumekuwa tukiendesha mafunzo hayo kwa kuleta wataalam kutoa mafunzo  hapa nchini  badala ya kutumia gharama kubwa kuwapeleka wataalam kupata mafunza bara la Ulaya na Marekani,”alibainisha.

Naye mkufunzi kutoka nchini Uingereza Dk Rick Brown alisema mafunzo hayo yatawasaidia washiriki  kutoa huduma bora na za kisasa za matibabu ya mifupa  hivyo ni furaha yao kuona Afrika inafanya vizuri katika matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles