25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MACHINGA COMPLEX ‘MFUPA MGUMU’

MAMII MSHANA Na LEONARD MANG’OHA

-DAR ES SALAAM

HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam, inatarajia kukabidhi jengo la Machinga Complex kwa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) uliendeshe baada ya kushindwa kurejesha mkopo waliochukua wakati wa ujenzi wa jengo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kufahamishwa kuwa deni na mkopo wa ujenzi wa jengo hilo la kibiashara umefikia zaidi ya Sh bilioni 40 kutoka Sh bilioni 12.7 zilizotumika wakati wa ujenzi wake.

“Halmashauri iliingia mkataba na NSSF wa mkopo wa Sh bilioni 10 za ujenzi wa jengo hilo, katika hatua za ujenzi mkataba huo ulifanyiwa nyongeza ya Sh bilioni 2.14 na kufanya jumla ya mkopo kuwa Sh bilioni 12.14, hata hivyo makabidhiano ya jengo hilo yalipofanyika mwaka 2010 gharama za ujenzi zilifikia Sh bilioni 12.7,” alisema Mwita.

Alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa hawana uhakika na uhalali wa deni hilo, ambalo lilipaswa kuwa la ghorofa tano kwa upande mmoja na sita kwa upande mwingine ambapo lingeweza kuhudumia jumla ya wafanyabiashara ndogo ndogo 10,000.

Mwita alisema jengo hilo limekabidhiwa likiwa na ghorofa nne huku likiwa na uwezo wa kuhudumia watu 4,206 pekee hali iliyosababisha halmashauri hiyo kushindwa kufikiwa malengo ya kulipa deni na kutoa huduma kwa walengwa.

Alisema halmashauri haikuhusika na usimamizi wa fedha zilizokopwa na kuifanya kushindwa kuthibitisha gharama zilizotumika.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa mkataba NSSF ilitakiwa kutoa fedha kwa halmashauri kwa ajili ya ujenzi jambo ambalo halikufanyika huku fedha ziliongezwa bila kuwapo makubaliano yoyote kati ya pande hizo.

“Kwa muda mrefu halmashauri imekuwa ikijaribu kutafuta mwafaka wa ulipaji wa deni hilo bila mafanikio,” alisema Mwita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles