24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

MABALOZI NCHI ZA KIARABU WAMSIFU JPM

Na MWANDISHI WETU – Dar es Salaam


BARAZA la Mabalozi wa Nchi za Kiarabu hapa nchini, limemsifu Rais Dk. John Magufuli na Serikali yake, juu ya msimamo wa kutounga mkono azimio la Marekani la kuutambua mji Mtakatifu wa Yerusalem kama makao makuu ya Israeli.

Limesema kuwa linathamini msimamo wa Serikali ya Tanzania wa kuungana na nchi nyingine 128 duniani ambazo zilipiga kura ya kupinga azimio hilo la Marekani katika mkutano wa dharura wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN), Desemba 21, mwaka jana.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na baraza hilo, imetanabaisha kwamba msimamo huo wa Tanzania unakwenda sambamba na msingi uliowekwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere wa kutambua haki za Mamlaka ya Palestina.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baraza hilo hapa nchini, limesema msimamo huo wa Tanzania unabebwa kwa thamani kubwa katika ngazi ya mataifa yote yanayotambua haki ya Wapalestina.

Mkutano wa dharura wa Baraza Kuu la UN uliokuwa na kaulimbiu ya “Matendo ya Israeli yasiyo ya kisheria juu ya Yerusalem ya Mashariki pamoja na ardhi ya Palestina inayokaliwa kimabavu”, ulilenga kutafuta azimio la pamoja la UN dhidi ya uamuzi mpya wa Serikali ya Marekani kuhusu mji wa Yerusalem.

Katika mkutano huo, nchi 128 zilipiga kura ya kupinga uamuzi wa Marekani wa kuutambua mji wa Yerusalem  kama Makao Makuu ya Israeli, huku Marekani ikiungwa mkono na nchi tisa pekee.

Kwa muktadha wa kura hiyo ambayo haifungamani kisheria, imeitangaza hatua ya Marekani kuhusu Yerusalem kuwa batili, na iliungwa mkono na mataifa mengi, matokeo ambayo yanaipa ushindi Palestina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles