26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Maajabu ya watekaji waliomrudisha MO

Na Waandishi Wetu, DAR ES SALAAM


WINGU zito bado limetanda juu ya aina ya watu waliomteka mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’, kisha kumwachia kwa kumtelekeza usiku wa manane wa kuamkia jana viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam.

Watekaji hao ambao bado hawajanaswa na vyombo vya dola, namna walivyomrudisha Mo na hata kufika katika eneo hilo la Gymkhana ambalo lipo katikati ya Jiji la Dar es Salaam, ni jambo ambalo tayari limezua mjadala.

Eneo la Gymkhana alilotelekezwa Mo mbali na kuwa karibu na ufukwe wa Bahari ya Hindi, hatua chache zipo ofisi zake, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Wizara ya Mambo ya Ndani, ofisi nyeti za ubalozi, mashirika ya kitaifa na kimataifa, hoteli na majengo makubwa yanayoaminika kuwa na kamera za usalama.

Ujasiri wa watekaji hao kumwachia Mo katika eneo hilo na kisha kulitelekeza gari lile lile walilotumia kumteka, lakini likiwa limebadilishwa namba za usajili, pia umezua maswali.

Juzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro wakati akitoa ripoti ya kwanza ya uchunguzi kuhusu tukio hilo, alisema watu waliomteka Mo walitumia gari aina ya Toyota Surf lenye namba za usajili AGX 404 MC ambalo alionesha picha zake na zaidi akisisitiza kuwa vijana wake hawatalala kwa kazi ya kuhakikisha mfanyabiashara huyo anapatikana.

Gari hilo ndilo hilo hilo lililomtelekeza, lakini likiwa …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles