27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MAADILI SIYO KWENYE KAZI ZA SANAA PEKEE, HATA KATIKA MAISHA BINAFSI

baraka-da-prince

Na JOSEPH SHALUWA

MSEMO wa msanii ni kioo cha jamii haujaanza leo. Hata maana yake haiwezi kuisha asilani katika maisha yote ya binadamu.

Ndiyo! Msanii ni kioo cha jamii, kwa sababu kupitia kazi zake watu watajifunza. Miongoni mwa kazi za sanaa ni kuelimisha jamii, kuburudisha, kuonya nk, hivyo ni jambo ambalo haliwezi kukwepwa kwa namna yoyote ile.

Inapotokea msanii anafanya mambo yasiyofaa jamii hushangaa, maana kupitia wao hupaswa kujifunza vitu vya maana kutokana na mafundisho yao.

Lakini wasanii wa kileo wamekuwa na tabia za hovyo kabisa. Ni baadhi ya wasanii, sina maana ya kwamba ni wasanii wote. Nazungumzia wasanii hawa wa kizazi cha sasa – muziki, filamu nk.

Baadhi ya video zao huwezi kuzitazama ukiwa na familia yako nyumbani au watu ambao unawaheshimu. Ni tatizo. Lakini jambo la kushukuru ni kwamba Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) hivi sasa wamekuwa wakali kwa wasanii ambao kwa namna moja ama nyingine wanaharibu maadili kwa kutoa video zisizo na heshima.

Pamoja na hayo, bado kuna tatizo kwenye maisha binafsi ya wasanii wetu. Kwenye video zao wanaweza kuwa makini kutokana na uangalizi mkubwa unaofanywa na chombo hicho cha sanaa, lakini kwenye maisha binafsi ni tofauti.

Hapo msanii anatakiwa kujitathimini peke mwenyewe, ajiulize: Je,  namna anavyoishi kunaakisi usanii wake? Je, jamii ina jambo lolote la kujifunza kupitia mavazi yao?

Wasanii mnatakiwa kujiheshimu, mjitambue kuwa mtazamwa na jamii nzima na hasa watoto na vijana ambao baadhi yao huwa na ndoto za kuwa wasanii hapo baadaye.

Ni aibu kwa msanii wa kike mwenye mashabiki wengi, kupita mitaani na mavazi ambayo hayana heshima. Ukiacha hayo, kumbuka kwamba una wazazi na ndugu wengine ambao unawawakilisha kupitia mavazi yako.

Ushauri wangu wa bure kwa wasanii wetu ni kujitambua na kuacha na kuiga mambo ya Wazungu ambayo hayana maana.

Kwani usanii lazima kujiachia hovyo? Kuvaa nusu utupu? Siyo sawa. Ni wakati wa wenye tabia hizo kuacha mara moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles