28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

Ma-DED wateule kuhakikiwa vyeti kesho

Rais Dk. John Magufuli.
Rais Dk. John Magufuli.

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

WAKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji, Manispaa na Wilaya, walioteuliwa  juzi na na Rais Dk. John Magufuli, wametakiwa kuwasilisha nakala halisi za vyeti vyao vya taaluma, kabla ya kuapishwa.

Zoezi la uhakiki wa vyeti hivyo litafanyika Ofis ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika jengo la Mkapa mjini Dodoma kesho kabla ya kuapa.

Wakurugenzi hao 13 ni pamoja na Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Manispaa mmoja, Mkurugenzi wa Mji mmoja na Wakurugenzi wa  Halmashauri za Wilaya 11, ambao wanatakiwa kuwasili Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma  kesho saa 2 asubuhi kwa ajili ya uhakiki wa vyeti vyao vya taaluma.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (TAMISEMI),  Mussa Iyombe na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Rebecca Kwandu, inawataka wakurugenzi hao kuhakikisha wanawasilisha nakala halisi za vyeti vyao vya taaluma kwa ajili ya kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya kitaaluma, unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi yaani vivuli.

Wakurugenzi hao na maaneo wanayokwenda kwenye mabano ni Godwin Emmanuel Kunambi (Manispaa ya Dodoma), Elias Ntiruhungwa (Mji waTarime), Mwantumu Dau (Bukoba), Frank Bahati (Ukerewe), Hudson  Kamoga (Mbulu), Mwailwa Pangani (Nsimbo), Godfrey Sanga (Mkalama)  na Yusuf Semuguruka (Ulanga).

Wengine ni Bakari Mohamed (Nachingwea), Juma Mnweke (Kibondo), Butamo Ndalahwa (Moshi), Waziri Mourice (Karatu) na Fatma Latu (Bagamoyo).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles