28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

LWANDAMINA APATA TIBA YA MBEYA CITY

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, ameanza kusaka mbinu za kupata ushindi mnono katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City, utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Lwandamina alionekana kutilia mkazo namna ya kuvuna mabao mengi katika michezo ijayo kuanzia wa Mbeya City kwa kuwanoa safu ya ushambuliaji waweze kufunga kwa kutumia kona na faulo.

Hadi sasa Yanga katika michezo tisa waliyocheza katika ligi hiyo, wamefunga mabao 11, wakati watani wao wa jadi, Simba, wamefunga mabao 21.

Kutokana na hali hiyo, Lwandamina ameona ni vema kutafuta njia zaidi za kuwawezesha kupata mabao zaidi ili kuwafikia wapinzani wao hao na kuepuka kukosa ubingwa kwa kuzidiwa kwa mabao kama ilivyokuwa msimu uliopita, walipowazidi watani wao hao kwa mabao baada ya kulingana pointi.

Katika mazoezi ya jana, Lwandamina alihakikisha kila kona inazaa bao, kama ilivyo kwa mipira ya faulo.

Hata hivyo, kwa upande wa mabao ya faulo, timu hiyo imevuna mabao mawili yaliyofungwa na Ajib, lakini ikipata bao moja tu kutokana na mpira wa kona.

Wachezaji hao walifanya zoezi hilo huku wakiwa wanarudia mara kwa mara katika upigaji wa faulo pamoja na kona, ili kupata urahisi wa kufunga mabao mengi kwenye mchezo wao dhidi ya Mbeya City.

Katika mchezo uliopita, Yanga waliambulia suluhu dhidi ya Singida United, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Namfua, Singida.

Yanga watawavaa Mbeya City wakiwa na kumbukumbu ya kuambulia kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza wa msimu uliopita, waliporudiana walishinda mabao 2-1 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga itawakosa nyota wake Donald Ngoma, Thaban Kamusoko, Amis Tambwe, Kelvin Yondan na Papy Tshishimbi, ambao ni majeruhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles