32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Lungu atetea kiti cha urais Zambia

Edgar Lungu
Edgar Lungu

LUSAKA, ZAMBIA

RAIS Edgar Lungu amechaguliwa tena katika uchaguzi wa urais wenye ushindani mkali, Tume ya Uchaguzi Zambia (ECZ) imetangaza jana.

ECZ ilisema Rais Lungu wa chama tawala cha Patriotic Front (PF) alipokea kura 1,860,877 sawa na asilimia 50.35 ya kura.

Mpinzani wake karibu mfanyabiashara Hakainde Hichilema wa chama cha upinzani cha United Party for National Development (UPND) alipata kura 1,760,347 sawa na asilimia 47.67 ya kura.

Wagombea hao wawili waliwaacha mbali wengine saba, ambao hakuna hata mmoja aliyefikisha zaidi ya kura 20,000.

Awali, UNPD ilijitangaza kujiondoa katika shughuli ya kuhakiki kura akidai uwapo wa udanganyifu huku ombi lake la kurudiwa kwa zoezi lakuhesabu kura katika baadhi ya wilaya likikataliwa na tume ya uchaguzi.

Hata hivyo, Hichilema ambaye amemshutumu Lungu kuharibu uchumi aliwaambia wanahabari kuwa chama chake kinataka kura zihesabiwe upya katika mji wa Lusaka kwa lengo la kuwa na uchaguzi, huru na wa haki.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya uchaguzi nchini humo tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, mshindi alihitaji asilimia zaidi ya 50 ya kura ili kuepuka uchaguzi wa marudio.

Mchakato wa kuhesabu kura baada ya kufanyika uchaguzi Alhamisi iliyopita ulichelewa na kusababisha upinzani ulalamike uwapo wa wizi wa kura, huku waangalizi wakitoa mwito wa utulivu.

Uchaguzi huo ulitanguliwa na kampeni kali zilizotawaliwa na mapigano ya mitaani, ijapokuwa wakati wa siku ya upigaji kura kulikuwa na utulivu.

Lungu, ambaye aliingia madarakani Januari 2015 baada ya kifo cha Rais Michael Sata, alishinda katika uchaguzi wenye ushindani mkali dhidi ya Hichilema mwaka jana.

Waangalizi wa kimataifa wametoa mwito wa utulivu na kuwataka Wazambia kuwasilisha malalamiko kuhusu mchakato wa uchaguzi mahakamani, badala ya kumiminika mitaani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles