27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Lulu arudi rasmi Instagram, awashukuru waliomuombea

Anna Potinus, Dar es salaam

Msanii wa filamu na maigizo Elizabeth Michael (Lulu), leo Novemba 16, 2018 ameweka ujumbe mzito wa maneno katika ukurasa wake wa Instagram baada ya kuwa kimya kwa zaidi ya mwaka mmoja tangu asomewe hukumu yake Novemba 13, mwaka jana.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwiwli jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba mwaka 2012, kabla ya kubadilishiwa adhabu hiyo na kuwa kifungo cha nje ambapo pia alifanya kazi za kijamii kuanzia Aprili hadi Novemba 10 mwaka huu.

Katika ujumbe huo Lulu amewashukuru wote waliomuombea katika kipindi hicho kigumu alichopitia na kwamba anaamini jaribu lolote ni kama mbegu na si tatizo kama wengi wanavyolichukulia.

“Ukipanda mbegu sehemu kubwa ya shamba lako na mavuno yatakuja kwa ukubwa uliopanda na ukipanda mbegu sehemu ndogo mavuno huja kwa kiasi ulichopanda,” ameandika.

Aidha ameandika kuwa lilikuwa ni jaribu kubwa, zito na la kuumiza na kwamba ni zaidi ya anachoweza kuandika au kueleza na kwamba mapenzi ya Mungu yametimizwa.

“Ilikua ni kikombe tu ambacho ni lazima nikinywe, yalikua ni majaribu tu ambayo yalikua niyapitie, yalikuwa ni mapenzi ya Mungu na yametimizwa… bado yeye ni Baba yangu, Mungu wangu, msaada wangu, kimbilio langu na ataendelea kuwa hivyo siku zote,” ameandika Lulu.

Aidha, katika ujumbe huo, mastaa mbalimbali walichangia akiwambo muingizaji Aunty Ezekiel na mtangazaji Zamaradi Mketema ambao waliandika maneno ya kumtia moyo Lulu kwa aliyopitia.

Lulu anakuwa msanii wa kwanza wa filamu nchini kuhukumiwa na kutumikia kifungo jela.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles