BRASILIA, BRAZIL
RAIS wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva ameachana na azma yake ya kugombea tena wadhifa wa rais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Uamuzi huo unamwachia nafasi mgombea mwenza, Fernando Haddad na ulifikiwa baada ya mkutano wa chama cha wafanyakazi katika mji wa Kusini, mwa Brazil ambako Lula amefungwa jela tangu Aprili alipokutwa na hatia ya ufisadi.
Hilo limeifanya mahakama kumpiga marufuku kugombea tena urais wakati akitumikia kifungo cha miaka 12.
Haddad, meya wa zamani wa Mji wa Sao Paolo ambaye pia alikuwa Waziri wa Elimu wa Serikali ya Lula ana chini ya mwezi mmoja kujinadi kwa wapiga kura kabla ya uchaguzi.
Mgombea mwenye sera kali za kibaguzi, Jair Bolsonaro ambaye alishambuliwa majuzi kwa kudungwa kisu tumboni wakati wa kampeni, ndiye anaongoza katika kura za maoni.