30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Lukuvi atishia kuvirudisha serikalini viwanja 6,000 vilivyotelekezwa

Veronica Romwald, Dar es Salaam

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ametishia kuvirudisha serikalini viwanja 6,000 ambavyo wamiliki wake hawajulikani na wametelekeza hati zao wizarani.

Aidha, amewaagiza maofisa ardhi wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam kufuatilia wamiliki hao kwani serikali imekuwa ikikosa mapato yatokanayo na kodi za viwanja hivyo.

Lukuvi ametoa agizo hilo leo Alhamisi Novemba 29, wizarani hapo alipozungumza na maofisa hao.

“Hati hizo 6,000 ambazo wenyewe hawajaja kuzichukua zipo tu hapa wizarani, nimewaagiza maofisa kuzikagua kiwanja baada ya kiwanja tuwajue wamiliki wake ni kina nani.

“Kwa sababu zipo hapa na serikali haipati kodi ya ardhi, tunaamini baadhi ya wafanyakazi wa ardhi waliopima vile viwanja waliweka majina bandia, wasipojitokeza wenyewe tutavichukua viwanja vile na kuviuza tena,” amesema.

Lukuvi amesema hati hizo zimetolewa na wizara zaidi ya miaka 10 iliyopita lakini hazijachukuliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles