28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ney wa Mitego atoa msaada kwa mama lishe, wajasiriamali Manzese

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki maarufu Ney wa Mitego, ametoa msaada wa fedha za mtaji kwa wanawake zaidi ya 50 wafanyabiashara wakiwamo mama lishe na wajasiriamali wadogo katika Soko la Manzese jijini Dar es Salaam.

Ney ametoa msaada huo leo Alhamisi Novemba 29, alipotembelea soko hilo na kuzungumza na kinamama hao ili kufahamu changamoto zao katika biashara zao.
Msanii huyo amesema sababu kuu za kutoa mitaji kwa kina mama wa Manzese ni kwa sababu mama yake mzazi pia alikuwa akiuza chakula maeneo hayo.

“Kina mama wanajitahidi kufanya kila biashara, muda mwingi wanashinda juani ili watoto wao waende shule na kupata mahitaji yao muhimu.

“Ningeweza kwenda kutoa msaada huu kwingine ila nimekuja Manzese kwa sababu ni sehemu niliyokulia na mama yangu mzazi pia alikuwa mama lishe hapa amenikuza kwa biashara hiyo hadi leo watu wananifahamu,” amesema.

Aidha Ney amesema hatua hiyo itakuwa endelevu kwa miezi minne mfululizo na atajitahidi kuwasaidia mitaji wakina mama wengi kote nchini kadri atakavyoweza. Hata hivyo hakutaja kiasi alichotoa akisema ni siri yake na wajasiriamali hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles