29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

LOWASSA AWEKA WAZI MAZUNGUMZO NA JPM

Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa ameweka wazi mazungumzo yake na Rais John Magufuli huku akisisitiza kuendelea na dhamira yake ya kusimamia mabadiliko kupitia Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa) licha ya kushawishiwa kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Lowassa alikutana na Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, ambapo pamoja na mambo mengine hatua hiyo ilizua mijadala mbalimbali huku watu wakitafsiri kuwa huenda Waziri huyo wa zamani akarudi CCM hasa baada ya kunukuliwa akimsifu rais kwa utendaji wake.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Januari 15, Lowassa amesema kwenda kwake Ikulu kulitokana na mwaliko alioupata kwa kutoka kwa Rais Magufuli Januari 9, mwaka huu akimtaka kukutana naye siku hiyo hiyo kwa ajili ya mazungumzo jambo ambalo alilitekeleza.

“Ujumbe wa Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kwangu ulikuwa ni kunishawishi kutaka nirejee CCM suala ambalo sikukubaliana nalo na milimueleza rais kwamba uamuzi wangu wa kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema haukuwa wa kubahatisha.

“Baada ya Rais Magufuli kunieleza ujumbe wake, nilitumia fursa hiyo kujadiliana naye juu ya masuala mbalimbali likiwamo kutoheshimiwa kwa katiba na sheria unaohusisha kupotea kwa watu, kuvamiwa na kutishwa na kushambuliwa kwa viongozi wa kisiasa wa upinzani, ukiukwaji wa mkubwa wa haki za binadamu, uminywaji wa demokrasia na hali ngumu ya uchumi kwa wananchi, ni imani yangu kuwa rais atayazingatia haya na kufanyia kazi masuala haya kwa maslahi ya nchi yetu,” amesema Lowassa katika taarifa yake hiyo.

Pamoja na mambo mengine, Lowassa amesema yuko imara na madhubuti kuliko wakati wowote na hatayumba wala kuyumbishwa akiendelea na dhamira yake ya kuamini katika Chadema na kusimamia mabadiliko kupitia Ukawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles