Lowassa aionya Serikali

0
675

lowasaNA MWANDISHI WETU

ALIYEKUWA mgombea urais wa Chadema chini ya mwavuli wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa, amezitahadharisha mamlaka mbalimbali kuacha kuwaandama wafanyabiashara na wananchi waliokuwa wanaunga mkono vyama vya upinzani wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba, mwaka jana.

Lowassa ametoa tahadhari hiyo wakati akitoa salamu za Mwaka Mpya kwenye ibada ya shukrani iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Ushirika wa Monduli.

Alieleza kusikitishwa na vitendo vya vitisho vya kuwafuatafuata wale waliokuwa wakisaidia upinzani jambo ambalo amelipinga na kusema kuwa kila mtu ana uhuru wa kuchagua chama anachokipenda na kwa kufanya hivyo dunia itawashangaa.

Katika hatua nyingine, Padri Gervas Taratara kutoka Shirika la Kimisionari la Roho Mtakatifu alitoa tafakari ya mwaka mpya kwa kusisitiza umuhimu wa kutengeneza amani ya kweli katika kila nyanja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here