27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Liwiti kupata shule ya sekondari

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Wanafunzi wa sekondari kutoka Kata ya Liwiti ambao wamekuwa wakilazimika kwenda kusoma nje ya kata hiyo sasa watapata ahueni baada ya kujengwa kwa shule ya sekondari.

Hatua hiyo inafuatia baada ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kutenga Sh milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo itakayojengwa jirani na Shule ya Msingi Liwiti.

Akizungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika ofisi za Serikali ya Mtaa Liwiti, Diwani wa Kata ya Liwiti, Alice Mwangomo, amesema mafanikio hayo yanatokana na ufuatiliaji walioufanya wa mara kwa mara pamoja na wajumbe wengine wa kamati ya maendeleo ya kata.

Amesema pia zimetengwa Sh milioni 65 kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Msingi Liwiti na Sh milioni 30 za ujenzi wa ofisi ya walimu Shule ya Msingi Misewe.

“Tulisema wakati tunaomba kura kwamba tutajenga shule ya sekondari, wakati mradi utakapoanza mwenyeki wa mtaa atapita kuwaambia wananchi wote wa mtaa huo wajitokeza kuchangamkia fursa ya ajira,” amesema.

Diwani huyo amesema pia barabara kubwa ambayo inatoka Kata ya Vingunguti na kupitia Kata ya Liwiti – Kata ya Kisukuru na Kata ya Kimanga itajengwa kwa kiwango cha lami.

“Tulipita kwenye mitaa tulisema tunavyo vipaumbele lakini pia ilani ilituelekeza, tulisema tutashughulikia suala la afya kuhakikisha zahanati yetu ya mtaa ipo katika mazingira mazuri na inatoa huduma bora,” amesema.

“Zahanati inahitaji ukarabati mkubwa tulipambana sana mimi na kamati nzima ya maendeleo na hatimaye Serikali Kuu imetupa Sh milioni 50 kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa,” amesema.

Diwani huyo kesho atasikiliza kero za mwananchi mmoja mmoja ili aweze kunua matatizo yanayowakabiki wnanchi wake na kuchukua hatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles