26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Liverpool watapindua matokeo kwa Barcelona kesho?

BADI MCHOMOLO

MTOTO hatumwi dukani, ndio kauli ambayo inatumiwa na mashabiki wengi kuelekea mchezo wa kesho wa nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya pale Liverpool watakapo shuka dimbani kuwakaribisha Barcelona.

Hii ni wiki ya mwisho kwa miamba minne kuoneshana ubavu wao ili mbili ziweze kufuzu hatua ya fainali, wakati huo mbili zikisalia.

Wiki iliopita tuliona ushindani wa hali ya juu kwa timu hizo nne ambazo ni Ajax, Tottenham, Liverpool na Barcelona, lakini wiki hii kila mmoja ana lengo la kufuta makosa aliyoyafanya katika mchezo uliopita ili kujihakikishia anaingia fainali.

Liverpool vs Barcelona

Wengi wanasubiri kesho kuona nini kinaweza kutokea kwenye mchezo huu ambao Liverpool wanajiandaa na mbinu mpya za kutaka kupindua matokeo kwenye uwanja wa nyumbani.

Wiki iliopita tuliona Barcelona wakiutumia vizuri uwanja wa nyumbani Camp Nou huku wakishinda mabao 3-0, jambo ambalo linaweza kuwa ngumu kwa Liverpool kulifanya wakiwa nyumbani.

Liverpool wameruhusu mabao mengi ugenini na wao bila ya kupata bao, hivyo wanahitaji kufanya kazi ya ziada ili kuhakikisha wanalipa kisasi hicho na kuingia fainali.

Wakiwa na lengo la kutaka kurudisha mabao yote matatu, watakuwa na kazi ya kumzuia mshambuliaji hatari Lionel Messi hasiwezi kuwaadhibu tena baada ya kuwafunga mabao mawili peke yake kwenye mchezo uliopita.

Barcelona wao lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanalinda lango lao wasiruhusu kufungwa bao au wasifungwe mabao kufikia matatu, lakini huku wakifanya hayo watakuwa na jukumu la kutafuta bao la ugenini.

Barcelona hawana kazi kubwa ya kuwaumiza kichwa kwa kuwa waliweza kufanya hivyo wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani, kikubwa ambacho watakuwa wanakiangalia ni kuhakikisha wanamiliki sana mpira.

Hata hivyo kwa upande wa Liverpool wanatakiwa kujitoa muhanga kwa kiasi kikubwa kwa kufanya kila liwezekanalo ili kupata ushindi mnono.

Chochote kinaweza kutokea kwenye mchezo wa mpira wa miguu, Liverpool wanaamini wanaweza kupata matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani na kuingia fainali, wakati huo Barcelona wakiamini tayari mguu mmoja umeingia fainali kilichobaki ni kumalizia mchezo huo wa mwisho kesho.

Ajax vs Tottenham

Ajax ni timu ambayo imeshangaza wengi msimu huu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, imeweza kuwatoa vigogo kwenye michuano hiyo kama vile mabingwa watetezi Real Madrid pamoja na Juventus.

Kutokana na umoja wao wakiwa uwanjani, wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri na kuingia hatua ya fainali.

Katika mchezo wa awali ambapo Ajax walikuwa ugenini nchini Uingereza, waliweza kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani hao Tottenham, lakini ushindi huo kwao ulikuwa muhimu sana kwa kuwa walikuwa ugenini.

Kesho kutwa watakuwa nyumbani wakipata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wengi ambao watajitokeza kuwapa sapoti kutokana na kile wanacho kifanya.

Hii itakuwa mara ya nne kwa timu hizi kukutana, mara ya kwanza zilikutana Septemba 16, 19981 kwenye michuano hiyo ambapo Ajax walikuwa nyumbani kwenye mzunguko wa kwanza na kukubali kichapo cha mabao 3-1.

Mchezo wa marudiano ulipigwa Septemba 29, huku Ajax wakiwa ugenini walikubali kichapo kingine cha mabao 3-0 na kuondolewa kwenye michuano hiyo.

Wiki iliopita ilikuwa mara ya tatu wanakutana na Ajax kufanikiwa kushinda wakiwa ugenini, lakini msimu huu Ajax wanaonekana kuwa na umoja wa hali ya juu ambao umewasaidia hadi kufika hapo kwa kuwa wana kikosi cha ushindani.

Hivyo katika mchezo huo wa kesho kutwa, uishindani utakuwa mkubwa huku kila timu ikipambana kutafuta bao la ushindi, lakini Ajax hawapo tayari kupoteza wakiwa nyumbani, wakati huo Tottenham wakihitaji ushindi wa mabao 2-0 ili kusonga mbele au 1-0 ili kwenye kwenye mikwaju ya penalti kwa kuwa kila timu itakuwa imeshinda ugenini.

Sifa moja wapo ya Ajax ni kushambulia kwa pamoja na kurudi kukaba kwa pamoja, hivyo inawafanya wachezaji wa timu hiyo waonekane wapo wengi uwanjani katika kila eneo ambalo mpira upo, ushindani mkubwa utatawala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles