27.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

LHRC wamtetea Raia wa India “aliyebambikwa “kesi ya uhujumu uchumi

Mwandishi Wetu, Singida

Kituo cha sheria na haki za Binaadamu kimejitosa kumtetea Raia wa India aliyekuwa Meneja Mkuu,kiwa da cha mafuta cha Mountmeru Millers Ltd cha Singida, Thilak Kumar(37) ambaye anashitakiwa kwa kosa la kumwibia mwajiri wake sh 169.3 milioni baada ya kuondolewa shitaka la uhujumu uchumi.

Mtuhumiwa huyo  kabla ya kushitakiwa Kwa kesi ya wizi alikuwa ameshitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi ambayo baadaye yaliondolewa  baada ya kukaa Magereza zaidi mwaka bila shauri kusikilizwa ni Raia wa

Mkuu wa LHRC kituo cha Arusha, Hamis Mayombo amesema wanamtetea Raia huyo wa India baada ya kuomba msaada wa kisheria kwani hana ndugu Tanzania na haki zake za binaadamu zinakiukwa.

“Amefata taratibu kuomba tumsaidie na hadi sasa amefutiwa kesi ya uhujumu uchumi na yunaendelea na kesi nyingine ambazo chanjo ni mgogoro na mwajiri wake aliyemleta nchini,”amedai.

Kesi hiyo, leo katika mahakama ya hakimu mkazi Singida ambapo, Jamuhuri imeomba kuongezewa siku 60 ili kukamilisha ushahidi.

Mwendesha Mashitaka wa serikali Almachius Bagenda alitoa maombi hayo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Singida,Elimo  Masawe.

Bagenda amesema amewasilisha maombi hayo kutokana na hati rasmi ya maombi hayo kutoka ofisi ya Mkuu wa  Upelelezi Mkoa(RCO) wa Singida ambaye ameeleza Upelelezi haijakamilika.

Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Hamis Mayombo wa LHRC licha ya kukubaliana na maombi hayo alitaka haki za Mshitakiwa kuzingatiwa kwani Kesi imekaa muda mrefu bila kuanza kusikilizwa.

Wakili Mayombo aliieleza Mahakama kuwa kama hakimu atafuta Kesi hiyo katika hatua za awali Polisi tayari walikuwepo eneo la Mahakama kumkamata Tena na itakuwa ni mara ya pili kuachiwa na kukamatwa tena.

Hakimu Masawe alisema hajaridhishwa na maombi ya siku 60 kwani kabla ya maombi hayo ilielezwa kuwa faili ya kesi hiyo limeombwa na Mkurugenzi wa mashitaka (DPP).

Alisema Kwa kuwa shauri hilo limechukuwa muda mrefu kutosikilizwa na Kwa kuzingatia maombi ya wakili wa Utetezi Kwani hata kama akifuta shauri hilo mtuhumiwa atakamatwa Tena anaahirisha Kesi hiyo hadi Desemba 6,2021.

Katika Kesi hiyo namba 45/2021 mtuhumiwa huyo yupo nje Kwa dhamama na ameshindwa kurejea nchini kwake ambapo ana mke na watoto watatu kutokana na kunya’ng’anywa pasi za kusafiria na kunyimwa stahiki zake na kampuni ya Mountmeru iliyomleta nchini.
Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles