25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

LAPF yazidi kung’ara kwa utunzaji wa kumbukumbu

Jengo la LAPF
Jengo la LAPF

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MFUKO wa Pensheni ya Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) umepewa tuzo ya kuwa mfuko bora Tanzania katika utunzani wa kumbukumbu za hesabu zake kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Ofisa Habari wa LAPF, Rehema Mkamba, alipokuwa akizungunza na MTANZANIA katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba, vilivyoko Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Kutokana na hali hiyo, Rehema alisema kitendo cha LAPF kushinda tuzo hiyo ni kielelezo cha mfuko huo unavyofanya kazi kwa kuzingatia sheria na kuwajali wateja wake.

“Mfuko unajali na kutunza kumbukumbu vizuri na hali hii inathibitisha kuwa malipo ya wastaafu hupitia katika akaunti zao.

“Tuna mfumo wa malipo wa kisasa kabisa, kwani mstaafu akikaribia kustaafu, anachotakiwa kufanya ni kujaza fomu zetu mapema ili tarehe ya kustaafu ikikaribia fedha zake azikute katika akaunti yake.

“Kwa mfumo huu tulionao, wastaafu wanalipwa haraka, ingawa pia tuna mafao ya uzazi,” alisema.

Kuhusu maonyesho hayo ya Sabasaba, alisema wananchi wanatakiwa kuendelea kufika katika banda lao kwa kuwa watajifunza mengi na kujua umuhimu wa LAPF katika maisha yao ya kila siku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles