27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

LAMECK DITTO: BADILISHA MAUDHUI KWANZA ILI MASHABIKI WASIKUBADILIKIE!

ULIPOBADILI mwelekeo kutoka ‘Kemo’ ya kiugumu enzi zile ulipokuwa unaishi Mji Kasoro Bahari a.k.a Morogoro na kuamua kujikita kwenye Zouk la malavidavi, mashabiki walikupokea vyema na bado wako nawe uliposukuma damu zao kwa mikong’osio yako ya ‘Moyo Sukuma Damu’ badala ya mengine.

Lakini kwa sasa katika ‘Front’ yako ambayo ni kama umeiwahisha kwa haraka kabla moyo haujamaliza kusukuma damu, unajipa matumaini na kuhanikiza mabadiliko kwamba ‘Atabadilika’ ingawa wewe mwenyewe unahitaji kubadikika kwanza kwenye mtiririko wa ‘Back’ uliyotoka.

Siyo kwenye Kemo lakini hii ya sasa kwenye malavidavi maana ukisikiliza maudhui yako na mikong’osio yako ni kama unajaribu kudhihirisha uwezo kwa kupita njia mbadala ya kimo cha sauti na uimbaji wako.

Lakini kwa mweledi anakutambua kwamba bado hujabadilika kuweza kushawishi mashabiki wako, ni kama badala ya kula chungwa umeamua kula chenza ambalo ni tunda jamii mkabala na la awali.

Hiyo ni sawa na maharage yalivyo na undugu na kunde au mbaazi yaani ni mlemle. Hata ukiangalia maudhui yako kwenye kichupa chako kipya cha ‘Kubadilika’ wewe mwenyewe hujabadilika kutoka ‘Back’ yako ya kusukuma damu hadi sasa, kile kichupa cha kwanza kilizimikiwa kutokana na jinsi ulivyokiibua manake eneo moja mabadiliko tu ya engo ya kamera lakini mnyange mtamu alikinogesha pia yale mambo ya hospitali.

Lakini Ditto hiyo haimaanishi kuwa kila kichupa chako unachokiandaa kiwe katika maudhui yaleyale kwa muktadha wa mandhari ingawa sipingani kabisa na uwezo wako ninaamini una uwezo mkubwa wa kukonga kuliko tunaouona sasa ila tu labda ni masuala ya usimamizi.

Kwamba ni namna gani unaandaliwa kuwasilisha lakini pia usisukumwe na mahitaji ya mbinyo kwamba toa kitu kingine kabla ya muda ili mashabiki wakukubali manake hiyo huwagharimu wasanii wengi, kwani mara nyingi unapotafuta ‘kutoka’ ngoma ya awali unaiwekea nguvu kubwa lakini ukifanikiwa inakupa kujiamini kupitiliza, kisha utahisi ya pili utaigonga na kupagawisha kama ya kwanza lakini usipokuwa mwangalifu mambo huwa tofauti, wewe siyo wa kwanza kukutana na hali kama hiyo katika muziki.

Cheki mwenyewe hata hapa Bongo msanii anaibuka poa katika ‘Back’ kisha anatokota katika ‘Front’ manake anakuwa amejipa makonfidensi kupitiliza, kumbe umakini ndiyo unatakiwa ingawa kwako bado ndiyo kwanza umeanza kutudhihirishia mauwezo yako kwenye kutiririsha mavoko yanayogusa mtima.

Kwahiyo hadi sasa iko poa japo pia haijafikia levo ya uwezo uliojificha ndani yako, fungukia mistari tukosome poa kisha utajikita mahala ambapo hakuna atakayekugusa kwani hata mikong’osio unayokita wasanii wengi ni kama wameitosa kwenye Bongo Fleva labda pengine iliwashinda au ‘walihit’ kwenye ‘Back’ wakaishiwa maarifa kwenye ‘Front’ ikawa mgando kama maziwa mbadala ya mtindi.

Kwa hiyo? Weka mambo tuone uwezo wako tukisubiri ‘Front’ nyingine manake inaelekea unawakonga Wabongo kwa voko yako iliyonyooka kwa kimo cha kupanda na kushuka, pengine itawavuta wengine nao wajikite kwenye Zouk za malavidavi ya malalamiko ya kuhanikizwa migubiko ya zero distance.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles